LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA AGOMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhiri Nkurlu, akipanda mti katika moja ya magati ya maji katika kata ya Bulinge wilayani humo muda  mfupi kabla ya kuondoka.
Shaban Njia
MKUU wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu juzi amegoma kushiriki maadhmisho ya kilele cha  wiki ya maji kiwilaya katika Halmashauri ya Msalala kwa madai ya kuwa hakukuwa na maandalizi ya kuridhisha.

Nkurlu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo alisema kuwa ya maazimisho hayo yalikuwa  hafifu huku ratiba ya sherehe hiyo ikiwa haijulikani wapi inaanzia na wapi inaishia hali iliyopelea kulazimika  kuendelea na ratiba nyingine za kazi za Serikali.

Maadhimisho hayo ya wiki ya maji katika Halmashauri ya Msalala yalifanyika katika kata Bulige  muda mfupi baada ya mkuu wa wilaya kuwasili katika maadhimisho hayo katika kata hiyo  iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya kuadhimisha sherehe hiyo ya wiki ya maji nchini.

Katika kuadhimisha sherehe za wiki ya maji kitaifa katika halmashauri ya msalala lengo ilikuwa ni kupanda miti katika vyanzo vya maji pamoja na maeneo ya magati ya maji sambamba na kuwakumbusha wananchi wa kata ya bulige umuhimu wa kutumia maji safi na salaama.

Fadhiri Nkurlu alisema kuwa hawezi kuendelea kuadhumisha sherehe hiyo huku magati ya maji hayatoi maji na kuongeza hawazi kufungua maghati ya maji huku maji yakitokchotwa katika maeneo mengine kwa ajili ya kufanikisha shughuli za upandaji wa miti katika maghati hayo.

“Ndugu mwandishi wa habari kwa hali hii wewe utaandika nini? Ratiba haijulikani nakila gati la maji tunalokwenda kupanda miti  hakuna maji ,sherehe za maji ili ziadhimishwe vizuri zinaambatana na maji kutoka katika vyanzo vya maji vilivyopo katika eneo husika la tukio.”alisema.

Nae makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Benedictor Manwari aliyechaguliwa kuwa mgeni rasmi muda mfupi baada ya Mkuu wa Wilaya kuondoka na kuendelea na majukumu mengine alisema kuwa Mkuu wa wilaya siku zote huwa anakwenda kwa muda nakuongeza kuwa siku nyingine kama tutakuwa na sherehe hizo tujitahidi kukamilisha ratiba kwa wakati.

Hata hivyo aliwataka wananchi wa kata ya Bulige kujitokeza kwa wingi pindi serikali ya kata inapotoa taarifa juu ya ugeni kutoka wilayani ama mkoani hali ambayo inafanya shughuli kumalizika kwa haraka na kisha kuendelea na shughuli nyingine.

“wanabulige tujitahidi sana kuwa tunaitikia wito toka serikali za kata zetu,taarifa hizi za ujio wa Mkuu wa Wilaya mlikuwa nazo siku moja kabla ya maadhimisho haya,chakushangaza tunafika hapa hakuna maandalizo yoyote yale na ikumbukwe mkuu wetu anakwenda kwa muda na nikwasababu anamambo mengi”alisema Manwari.

No comments:

Powered by Blogger.