LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWILI WA MAREHEMU MTONGORI MANG'ACHE WAAGWA JIJINI MWANZA.

Kulia ni mtumishi wa Mungu kutoka Kanisa la SDA Mabatini Jijini Mwanza, akiongoza ibada ya kuuaga mwili wa marehemu, Mtongori Mang'ache, hii leo jioni March 03,2017. Kushoto ni ndugu, jamaa na marafiki akiwemo Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
#BMGHabari

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Koplo Thomas Binagi Mang'ache (wa kwanza Julia wanaume waliokaa).
Marehemu Mtongori Mang'ache enzi za uhai wake.

Ibada ya kuuaga mwili wa shangazi yetu mpendwaMtongori Mang'ache, imefanyika hii leo jioni nyumbani kwa kijana wake, Koplo Thomas Binagi Mang'ache, Mabatini Jijini Mwanza.

Mwili utasafirishwa kesho jumamosi saa mbili asubuhi kwenda nyumbani Tarime kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho kutwa jumatatu.

Marehemu alizaliwa mwaka 1932 Tarime mkoani Mara na hadi mauti yanamkuta jana 02.03.2017 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza, alikuwa na umri wa miaka 85.
Bwana alitoa, Bwana ametwaajina lake lihimidiwe, Amina!

No comments:

Powered by Blogger.