LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAMKO LA OJADACT KUHUSU TUHUMA ZA MAKONDA KUVAMIA STUDIO ZA CLOUDS.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

PRESS  CONFERENCE                  OJADACT                               MACHI 23, 2017, CCM BUILDING 
Maudhui:  Uhuru wa  Vyombo vya  Habari na Usalama wa Vyombo vya Habari.

NDUGU   Waandishi wa Habari, Chama  cha Waandishi wa Habari wa Kupiga   Vita  Matumizi ya  Dawa za Kulevya  na Uhalifu Tanzania (OJADACT), leo hii  tumewaita  hapa  kuzungumza  nanyi  juu  ya  mwenendo wa    Uhuru wa  Vyombo  vya  Habari Nchini  na  usalama wa Vyombo vya  Habari  na Waandishi  wenyewe.

Waandishi,  OJADACT  imefuatilia  kwa ukaribu tangu  litokee  sakata  la  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  kuvamia  kituo cha  Clouds  media  na  kubaini  mambo  mbalimbali , ambayo  leo  tumeona  tuyatolee  ufafanuzi  zaidi.

Kwanza  kabisa, OJADACT  tunakili  wazi  kuwa,  hali  ya  uhuru wa vyombo vya  habari Nchini  sio nzuri kwa sasa, licha  ya kuwepo  kwa  sheria  mbalimbali  mbaya  hapa  Nchini, bado mwendelezo  wa kuvinyanyasa  vyombo  vya  habari  kupitia  wateule wa Rais  imeendelea.

OJADACT, tunalaani  kitendo  hicho kama taasisi  nyingine   zilivyofanya  ,pia   kwa  ushauri  wa  vyombo  vya  habari    tunapendekezo  yafuatayo;

*Vyombo  vya  habari  vihakikishe  vinakuwa  na    ulinzi  wa kutosha  kwenye  vituo  vyao  ili  kuzuia  uvamizi wa  watu  wasio  na nia  njema   na  vyombo vya  habari.

*Vyombo  vya habari viepuke   kuwa  na  urafiki wa  jirani na wanasiasa na viongozi wa Nchi, kwa kuwa,  kufanya  hivyo  kunaweza   athiri  operesheni  za  vyombo   vya  habari  pale  vinapoonekana  kuwakwaza watawala.

*Vyombo  vya  habari  vizingatie  sheria  ya  huduma  ya  vyombo vya  habari  ya  kuwa  na watendaji   wenye  weledi wa kitaaluma  ili  kuitendea  haki  taaluma kwa kutopokea maelezokez

*Vyombo  vya  habari  visiruhusu  vyanzo  vya  taarifa  (sources)  kuwa  sehemu  ya  kutengeneza maudhui  ya   habari, wajibu  huo waachiwe  wahariri wa  vyombo  vya  habari.

*Mahusinao  ya vyombo   vya  habari  na  wadau  yawe  na  mipaka  ili  kuepusha  mgongano wa maslahi  kwenye  zoezi  la  uchakataji  wa habari.

*Serikali    iheshimu  uhuru  wa habari  hapa Nchini  ili vyombo   hivyo  view  chanzo  cha   kuleta  maendeleo.

*Tunampongeza  aliyekuwa waziri wetu wa habari Nape  kwa maamuzi  yake  ya  kuitetea  tasnia.

Edwin Soko
Mwenyekiti, OJADACT

No comments:

Powered by Blogger.