LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIONGOZI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WAHIMIZWA KUWA MABALOZI WEMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 James Salvatory, Dar
Viongozi wa dini na madiwani wa ManiSpaa ya Ilala wametakiwa kuwa mabalozi wazuri kwa kuhakikisha wanaelimisha wananchi kutoharibu miundombinu ya gesi na badala yake wailinde kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo  jijini Dar es salaam na mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema  wakati akizungumza na viongozi hao katika semina ya mradi wa gesi asilia iliyoandaliwa na shirika la maendeleo ya petroli nchini(TPDC)kwa kushirikiana na kampuni Tanzu ya usambazaji wa gesi wa shirika hilo GASCO kuwaelimisha na kuwajengea uwezo juu ya mradi wa huo.

Bi Mjema amesema kuwa kama wananchi wataelimishwa kuepuka kufanya matukio yanayohatarisha miundombinu ya gesi asilia ikiwemo ile inayotoka Songosongo na Mtwara hali hiyo itaifanya miundombinu hiyo kuwa salama na hatimaye wananchi kuweza kufaidika na nishati hiyo.

Kwa upande wake kaimu meneja mkuu wa kampuni Tanzu ya TPDC (GASCO) Rodrick Moshi amesema kuwa shirika hilo litaendelea na mpango wake wa kuhakikisha mradi wa gesi asilia unakuwa rafiki kwa wananchi hivyo itaendelea kukutana na makundi mbali mbali ili kuhakikisha linatoa elimu juu ya mradi wa gesi kwani asilia 50%ya umeme unaozalishwa hapa nchini hutokana na gesi hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi na makundi mengine kuelimishwa kwa kina juu ya mradi huo.

No comments:

Powered by Blogger.