LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO WA CUF WAVAMIWA NA WATU WALIOKUWA WAMEFICHA SURA ZAO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

BlogRafiki
Watu wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. 

Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo. 

Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka. 

Mtu huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na wenzake katika eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi huo katika mkutano wa wanachama wa CUF. 

Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.

No comments:

Powered by Blogger.