LIVE STREAM ADS

Header Ads

MUBASHARA MATOKEO YA MBAO NA SIMBA CCM KIRUMBA.


Shabiki wa Simba kindakindani.

Judith Fedinand, Mwanza
Mbao wanapata goli kipindi cha kwanza dakika ya 21 mfungaji akiwa ni George Sangija.

Mbao wanapata goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Evarist Benard ikiwa ni dakika ya 36, kipindi cha kwanza.

Kipindi cha kwanza kinamalizika, sasa ni mapumziko. Mbao 2-0 Simba.
Ni kipindi cha pili, bado mpira ni piga nikupigie.

Gooooo gooooo goooooooo
Simba wanafunga goli dakika ya 88 kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Fredirick Blagnon.

Simba wanapata bao la pili dakika za nyongeza ikiwa ni dakika ya 92.
Go goooo gooooo Simba wanapata bao la tatu ikiwa ni dakika za lala salama. Simba 3-2 Mbao.

Pee pee peee mpira umekwisha, Simba wanatoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa tabu wa bao 3 dhidi ya 2 za Mbao.

No comments:

Powered by Blogger.