LIVE STREAM ADS

Header Ads

SARAKASI ZAENDELEA NDANI YA CUF.



James SalvatoryDar
Sarakasi zimeendelea ndani ya Chama cha Wananchi CUF, baada ya Mwenyekiti wake anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba kumshutumu Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif kwa madai ya kutaka kukiua chama hicho.

Profesa Lipumba alitoa tuhuma hizo juzi, wakati wa kongamano la Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvicuf), lililofanyika kwenye ofisi za chama hicho Buguruni Jijini Dar es salaam.

Akihutubia kongamano hilo, Profesa Lipumba alimtuhumu Maalim Seif kwa madai ya kubadili utaratibu wa vikao vya ushauri kwa kuzungumza na mkurugenzi mmoja mmoja badala ya kuwaweka pamoja na kusema kitendo hicho ni cha kumdhalilisha Naibu Katibu mkuu wa chama hicho Bara, Magdalena Sakaya.

Aidha alisema Sakaya amefanya kazi kubwa sana kukijenga chama hicho  Lakini bado Katibu Mkuu  kamsimamisha uanachama Sakaya ili afukuzwe ubunge.

Alisema huu ni wakati wa kukijenga chama na hakuna mwanasiasa bara aliyefanya kazi kubwa kuwatetea Wazanzibari kama yeye (Lipumba).

Hata hivyo, Lipumba alisema amemsamehe Maalim Seif na yupo tayari kukaa naye meza moja ili kukijenga chama hicho ikiwamo kujenga uchumi utakaoleta manufaa kwa wananchi Wakati wowote Maalim Seif aje tuzungumze na turekebishe mambo.

Pia, Lipumba alikishutumu Chama cha Chadema kwamba kinamhadaa Maalim Seif na kinaweza ‘kumuuza’ kama kilivyofanya kwa Dk Wilbrod Slaa na kwamba hakina demokrasia kama kinavyotamba.

No comments:

Powered by Blogger.