LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT YABAINI CHA ONGEZEKO LA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for EDWIN SOKONa Nelson  Emmanuel,Mwanza 
Chama  Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga  Vita Vita  Matumizi  ya Dawa  za  Kulevya  na  Uhalifu   Tanzania (OJADACT), kimesema ukosefu wa  elimu  ya  athari za dawa za kulevya   kumechangia  kwa  kiasi  kikubwa  ongezeko  la  matumizi  ya  dawa  za kulevya  Nchini. 

Akiongea  mbele  ya  Waandishi wa  habari mapema Jijini Mwanza, Mwenyekiti wa  OJADACT, Bwana  Edwin Soko, alibainisha   kuwa, jamii   haina  uelewa  wa  athari za dawa za kulevya    hasa  kwenye  athari  na  ndio maana    vijana  wengi wameingia  kwenye  matumizi  ya dawa  hizo bila  kujitambua.

“ Utakuta  mtu anatumia  dawa za kulevya  kwa  dhamira  ya  kutaka  kuonja  zinafafanaje  na kuamini  kesho  yake  hata  tumia  dawa  za kulevya, lakini  kumbe  hajui  dawa  za kulevya  hazionjwi” Alisema Bwana  Soko.

OJADACT, imesisitiza    utoaji wa  elimu  juu  ya    dawa za kulevya  uzingatiwe  na kupewa  umuhimu  kwenye taasisi  za  makundi  ya  vijana  kama  vyuoni  na  sehemu za michezo  ili  kunusuru  Taifa  kuendelea  kuwa  na   idadi  kubwa  ya watumiaji wa dawa z akulevya.

Bwana  Soko, aliongeza kuwa, kwa sasa  OJADACT  wamekuwa na  kampeni  ya  kuwahamasisha  vijana   kwenye  mfumo wa kupata  elimu juu  ya  dawa za kulevya  kupitia  michezo  mbalimbali  inayoendelea Nchini,  kwani michezo  ni sehemu  ya  kujenga   afya  na  kupeana  elimu  juu  ya  afya.

Moja  ya  athari za  dawa  za kulevya  kwa   mujibu wa  bwana Soko, ni kuathirika kiafya, kimwili na kiroho, ambapo  mtu  anayepata  athari  zote  hzio  uwa  ni ngumu sana  kukubalika  ndani  ya  jamii, ni  wazi  sasa  jamii  lazima  ichukue  hatua  kupiga   vita  matumizi ya  dawa za kulevya. 

No comments:

Powered by Blogger.