LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA AMANI GIRLS LAWANOA WACHAMBUZI WA SERA JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Nelson Emmanuel,Mwanza 
Shirika  la  Amani   Girls Jijini Mwanza,   limeendesha  zoezi  kwa  uchambuzi wa  sera mbalimbali Tanzania  ili  kuweza  kuwasaidia  watu  wanaoishi  na  Virusi vya Ukimwi  Tanzania  wapatiwe  huduma  bora za  afya  kwa lengo  la  kuboresha  afya  zao.

Wiki hii shirika  hilo   limefanya  uchambuzi wa  sera ya  vijana  kutazama  jinsi  inavyotoa   kipaumbele   kwa  vijana  katika  kupata  huduma za  vitu mbalimbali  kama  kuwezeshwa  kiuchumi, sera  ya   jinsia wanawake  kwa  lengo  la kutazama    vipaumbele  na  utekelezwaji wa   haki za wanawake  Nchini.

Naye  Mwezeshaji   Pentaleon  Shoki  aliwaeleza washiriki  umuhimu wa  kupitia  sera hizo  ni  mkubwa,  kwani zinawasaidia   mabinti  kujielewa  na  kutambua  vipaumbele  kwa  ajili ya  kujitambua  na  kupata  haki  zao  za msingi.

“Tunaweza  kuwa na  sera  nzuri  lakini   tatizo  likawa  ni kwenye  utekelezaji wa sera hizo na kusababisha    jamii   kuishi  kwenye maisha  ya umaskini  yanayoweza kuathiri   afya  zao  na kushindwa  kuchangia  falsafa  ya  viwanda kwenye  kuufikia uchumi wa kati.

Naye  Mshiriki wa  wa mafunzo hayo  Bwana  Edwin Soko  alisema  kuwa, mafunzo hayo  ni muhimu kwa  vyombo vya  habari  kushiriki kikamilifu  kwenye  zoezi  la  uchambuzi wa  sera  ili  viweze  kufikisha  ajenda ya haki  kwa wanawake  mbele  ya  jamii.

“Vyombo  vya habari  vina  nguvu sana  hivyo  basi  kushirikishwa  kwenye  chambuzi wa sera  ni jambo  muhimu  kwani  vitaweza  kusaidia  mapambano  ya  kumpigania  mtoto  wa  kike  kwenye  kupata  haki zao”  Alisema Bwana  Soko.

Mafunzo  hayo  yalikuwa ni  ya siku  moja  na kuhusisha wataalamu wa  sera takribani    ishirini  na  yalifanyika  kwenye  hotel  ya  Adden  Palace.

No comments:

Powered by Blogger.