LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIMBA YATUMA SALAMU KWA MBAO FC.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Timu ya Simba ikifanya mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na timu ya Geita Gold Sport Mchezo ambao umechezwa kwenye shule ya msingi ya Waja.

Timu ya Geita Gold Sport akijiweka sawa kucheza mchezo wa kirafiki na Simbo.

Timu zote mbili zikiingia uwanjani kukabiliana.


Mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba.


 Mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Geita Gold Sport. Mchezo   wa kirafiki  baina ya simba Sport club  na Geita Gold sport  ya Mkoani Geita umemalizika kwa timu ya simba kuifunga Geita gold mabao 7-0, ambapo wekundu hao wa msimbazi wamelilipiza kisasi kutokana na mchezo wao wa kirafiki mwaka jana ambapo simba walichezea magoli matatu kwa moja.

Ushindi huo umetokana na mabao ya viungo Said Hamisi Ndemla, Pastory Athanas, Mwinyi Kazimoto moja kila mmoja wakati Mohammed Ibrahim alifunga mawili sawa na mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagnon.

Simba imeweka kambi Geita ikitokea Bukoba, ambako Jumapili ilichapwa 2-1 na wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.


Na Wekundu hao wa Msimbazi wanajiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu, dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza wiki ijayo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

No comments:

Powered by Blogger.