LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAMBO ZA CHAMA CHA SOKA MKOANI MWANZA MZFA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Chama cha Soka Mkoa wa  Mwanza (MZFA), kimejipanga kutoa zawadi kwa timu itakayoibuka na  ushindi wa kwanza mpaka wa tatu katika ligi daraja la tatu mkoa.

Hayo yalisemwa  juzi na Katibu wa MZFA Charles  Malongo wakati    akitoa taarifa kwa waandishi wa habari namna ligi daraja la tatu mkoa inavyoendelea.
Malongo alisema, tangu ligi hiyo imeanza mpaka sasa hawajapata  wadhamini,hivyo kama mkoa wamejipanga kutoa zawadi kwa timu itakayoibuka mabingwa msimu wa 2016/17, itakayo shika  nafasi ya pili na tatu,ili kuendelea kuhamasisha  wachezaji.

"Sisi kama chama cha soka mkoa tumejipanga kutoa zawadi kwa timu itakayo ibuka na ushindi msimu wa 2016/17 kwa kuwapatia kombe na fedha taslimu laki 3,itakayoshika nafasi ya pili itapatiwa laki mbili huku itakayo shika nafasi ya tatu watajinyakulia kitita cha shilingi laki mmoja," alisema Malongo.

Pia alisema, kutakuwa na timu bora ya ligi,hivyo aliwaomba waamuzi waendelee kuchagua wachezaji bora 11, ambao watasaidiwa na chama kuwaendeleza na kufika mbali kimichezo.

Hata hivyo alisema, katika ligi hiyo wamekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya waamuzi kushindwa kumudu sheria 17 za mchezo.

Aidha alisema, baadhi ya waamuzi walipewa barua ya onyo akiwemo  Mbaraka Almas katika mchezo wa 7,akiwa muamuzi wa akiba alishindwa hakufika pia hakutoa taarifa yoyote, huku Paul Seleji kwenye mchezo namba 6, uliochezwa machi 13 mwaka huu, kati ya Mnadani Fc dhidi ya Kukimbiji,akiwa muamuzi wa kati alishindwa kujali afya za  wachezaji waliokua wanaumia,hivyo walimuhukumu kwa mujibu wa sheria namna 28 ya ligi mkoa daraja la 3.


Vilevile aliwaomba mashabiki kuwa watulivu na kushangilia katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya timu husika, na kutoingia uwanjani wakiwa wamelewa  sambamba na madereva kuendesha magari kwa ustarabu,kwa ajili ya usalama wa mashabiki na wachezaji.

No comments:

Powered by Blogger.