LIVE STREAM ADS

Header Ads

TBS kuelimisha wafanyabiashara,mawakala mkoani Mwanza.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limewanoa wafanyabiashara na mawakala kutoka mkoani Mwanza,wanaoagiza bidhaa nje ya nchi,namna ya kusimamia na kuagiza bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora na kufuata taratibu,kanuni na sheria  ya viwango namba 2 ya  mwaka 2009.

Elimu hiyo ilitolewa jana katika semina iliyoandaliwa na TBS, yenye lengo la kuwaelimisha waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na mawakala wa forodha Kanda ya Ziwa,iliyofanyika katika ukumbi wa jiji la Mwanza.

Akizungumza katika semina hiyo Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Ubora(TBS) Ridhiwani Ramadhani aliwaomba washiriki wa mafunzo hayo,kutumia elimu walioipata ili kufuata utaratibu wa uagizaji bidhaa, kama ilivyo katika kanuni na sheria ya viwango inavyoelekeza,kwa ajili ya kuendelea kibiashara na kuepuka  usumbufu wa faini.

Ramadhani alisema, jukumu la shirika hilo ni kuhakikisha bidhaa zinazoingia sokoni zina ubora,usalama wa afya ya wananchi na mazingira,kwani licha ya wao kuwa wakaguzi na wasimamizi pia ni walaji, hivyo ni wajibu kutoa elimu kwa wadau.

Pia alisema, serikali.  ilifanya makubaliano na Shirika la Ubora nchini  China,kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini kutoka kwao zinakidhi viwango vya ubora,hii ni kutokana na malalamiko yaliyopo ya kuwa,wanaleta bidhaa ambazo kiwango chake ni cha chini.
Kwa upande wake Afisa Mdibiti Ubora Kanda ya Ziwa Joseph Makene alisema, changamoto wanazokubana nazo ni pamoja na baadhi ya waagizaji kutokuwa waaminifu kwa kufoji nyaraka,kuingiza bidhaa kwa njia zisizo sahihi na kuwatumia maofisa ambao siyo waadilifu.

Aidha alisema,kushamiri kwa biashara ya bidhaa zilizotumika inachangia kufanya udhibiti ubora unakuwa mgumu sambamba na uhaba wa wafanyakazi.

Hata hivyo aliomba ushirikiano kutoka kwa wafanyabiashara na taasisi zingine,ili kusaidia nchi yetu kutokua jalala la bidhaa.
Naye Mkurugenzi wa ZARA Solar mkoani Mwanza Mohamed Parpia aliiomba TBS,ielekeze wafanyabiashara viwango vinavyohitajika,ili wasiweze kupata hasara na kuepuka faini na usumbufu.

Vilevile mmoja wa washiriki wa semina huyo Charles Nobat alisema, shirika hilo linatakiwa kujenga maabara mkoani Mwanza ya Mkemia Mkuu itakayotumika na mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kupima bidhaa, hali itakayosaidia kupunguza gharama kwa wafanyabiashara.

No comments:

Powered by Blogger.