LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau Wa michezo waliojitokeza kusambaza vifusi katika barabara iliopo nje ya uwanja wa CCM Kirumba.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Judith Ferdinand,Mwanza
Wadau wa michezo kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza, wameombwa  kuendelea kushirikiana na uongozi wa uwanja wa CCM Kirumba,ili kuboresha mazingira ya uwanja huo.

Wito huo umetolewa leo na Meneja wa uwanja huo Steven Shija wakati akizungumza na BMG, ofisini kwake jijini Mwanza.

Shija amesema,mazingira ya uwanja yakiwa bora yatasaidia kuendeleza  michezo na kuinua uchumi wa  mkoa huo,hivyo wadau wanatakiwa kushirikiana ili kufikia lengo.

"Uongozi wa uwanja  unaendelea kuwaomba wadau wa  michezo ndani na nje ya mkoa wa Mwanza, kuendelea kushirikiana na  sisi, ili  kuboresha mazingira ya uwanja wetu," amesema Shija.

Pia amewashukuru,wadau  waliojitokeza jana kwenye zoezi la kusambaza vifusi vya changarawe  katika barabara iliyoharibika nje ya uwanja huo.

Hata hivyo amesema,uongozi Wa uwanja huo unatoa pongezi kwa Mwanza Veterans  kujitolea kwa hali na mali kufanikisha upatikanaji wa vifusi vya changarawe pamoja na  usambazaji.

Aidha amesema, katika zoezi la usambazaji changarawe wadau mbalimbali walishiriki akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu  CCM Taifa, kutoka Wilaya ya Nyamagana Jamal Abdul Babu,Mwanza Veteran na uongozi wa uwanja.

No comments:

Powered by Blogger.