LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANA CCM WAASWA KUELEKEA KWENYE CHAGUZI ZAO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wameombwa kuchagua viongozi bora, watakaoendana na karne hii ya ushindani wa uhalisia na vitendo.

Ni katika uchaguzi  wa  chama hicho unaotarajiwa kufanyika mei mpaka desemba mwaka huu,wa kuwania  nafasi mbalimbali, kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa.

Wito huo umetolewa jana na Katibu CCM Mkoa wa Mwanza Raymond Mwangwala wakati akizungumza na BMG ofisini kwake jijini Mwanza.

Mwangwala alisema,wanachama ndio wanauwezo wa kuchagua viongozi,hivyo aliwaomba wasaidie chama kupata viongozi bora watakaoendana na karne hii ya ushindani ya kwenda kushindana  katika uhalisia na kutafsiri vitendo.

"Naomba wanachama wa CCM kutowapa kura wagombea watakao tumia rushwa, katika uchaguzi na kutangaza nia kabla ya muda,ili kupata viongozi bora na waadilifu wenye nia ya dhati ya kukipeleka chama mbele na serikali kwa ujumla sambamba na kutuvusha salama mpaka mwaka 2019,katika uchaguzi wa serikali za mitaa," alisema Mwangwala.

Pia aliwaomba  wanaccm kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na  kutumia demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa pamoja na kuhakikisha wanania ya dhati ya kutumikia chama na taifa.

Hata hivyo aliwaonya wale wote watakaotumia rushwa katika kipindi cha uchaguzi na kubainika hawatasita kumuondoa katika nafasi hiyo,sambamba na kuwataka wakajipime na wasiende kwa kutaka kutukuzwa bali  wakawatumikie wanachama na wananchi.


Aidha aliwaomba, watendaji wa chama hicho kuacha kukaa ofisini na badala yake washuke chini, kama anavyo fanya ili kuelimisha wanachama na kuangalia  mambo yanaenda kama  walivyopanga.

No comments:

Powered by Blogger.