LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAHIMIZWA KUSHIRIKI MASHINDANO YA TEHAMA JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Judith Ferdinand, Mwanza
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mkoani Mwanza, wametakiwa kushiriki katika mashindano ya Tehama, ili kuweza kutoa mawazo yao,kwa ajili ya kujipatia ajira na kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayokabili jamii na mkoa kwa ujumla.

Wito huo ulitolewa juzi na Mkurugenzi wa Ubunifu,Ujasiriamali na Ushindani kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt.Mafunda Bugushile katika mafunzo endelevu kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo tofauti mkoani hapa.

Bugushile alisema, kupitia mafunzo hayo,wamelenga kuwafundisha wanafunzi hao,kupenda kujitegemea wakiwa vyuoni na baada ya kumaliza masomo yao,kwa kuweza kutoa mawazo na kuyafanyia kazi kwa lengo la kuwasaidia wananchi na mkoa  pamoja na kuendelea kutatua matatizo bila usumbufu.

Naye Mkuu wa Kituo cha Ubunifu kilichopo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Jackline Dismas alisema, wanafunzi wa vyuo wana fursa kubwa ya kuyatumia mawazo yao,ili kuweza kuwasaidia katika kujiongezea kipato kwa kuweza kufungua  kampuni zao.

AliongezaMwanza
wataweza kutengeneza  ajira kwa vijana jambo litakalosaidia serikali pamoja na kuwaomba wasichana kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi kutoka Chuo cha Mount Meru (Mwanza) John Mayala ambaye ni mnufaika wa mafunzo hayo alisema, ameweza kufahamu namna ya kutumia utaalam katika teknolojia kwa kutafuta na kutengeneza wazo lake pamoja na kulifanyia kazi,ili mtu mwingine asiweze kutumia wazo lake na kulitumia kama lake.

Aidha Thea Mushi alisema, wapo sawa watu katika sekta ya maendeleo hakuna kumuacha nyuma mwanamke na mwanaume asonge mbele,hivyo wameelekezwa mambo ambayo walikua hawajui na wataenda kuyafanyia kazi.

Hata hivyo alisema, kupitia mafunzo hayo wamejifunza kuwa wanatakiwa kusoma kwa ajili ya kupata ujuzi na kujiajiri wenyewe na kucha kusubilia ajira kutoka serikalini.

Kadhalika wanafunzi wa vyuo ambao wamepatiwa mafunzo hayo kutoka jiji la Mwanza ni Mount Meru, Mtakatifu Augustine(Sauti), Dar es salaam Institute of Technology (DIT) Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.