Watanzania kunufaika na umeme wa jua, majiko bunifu ya SunKing
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Meneja Masoko wa kampuni ya SunKing nchini Tanzania, Albert Msengezi akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za SunKing nchini, uliofanyika hii Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Wakazi wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu inayosambazwa na kampuni ya Sun King.
Meneja Masoko wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi ameyabainisha hayo jijini Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo ni taa za sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.
“Kila Kijiji nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao watawafikia wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni Moja ambapo tumejikita kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo taa za sola na majiko yasiyochafua mazingira” alibainisha Msengezi.
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja na kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana aliwahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira zaidi kwa vijana.
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya SunKing Tanzania, Judie Wu akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza jijini Mwanza.
Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za SunKing nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
Mkuu wa Biashara wa kampuni ya Sun King, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya SUNKING mkoani Mwanza, Henry Mwayawale akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kitaifa. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia), akizindua ofisi ya SunKing Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kitaifa.
Mfanyakazi wa SunKing akitoa maelekezo kwa mteja ofisini.
Kampuni ya SunKing imetoa zawadi kwa wafanyakazi wake walioongoza kwa mauzo katika kipindi cha mwezi wa tatu.
Wachekeshaji wa Futuhi wakichekesha kwenye uzinduzi huo kuhusiana na bidhaa za SUNKING.
Wachekeshaji wa Futuhi wakisherehesha kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na wafanyakazi wa SUNKING wakifuatilia hafla hiyo.
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: