LIVE STREAM ADS

Header Ads

102.5 LAKE FM MWANZA WATINGA KWA WANANZENGO KUPITIA GULIO LA MTAA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi Mkuu wa Lake Fm Mwanza, Doreen Noni, akiwasilisha shukurani na salamu zake kwa niaba ya wafanyakazi wake kwenye burudani ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza.

#BMGHabari
102.5 Lake FM Mwanza, #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo jana Mei 26,2017 ilizindua rasmi burudani za Gulio la Mtaa kupitia kampeni yake ya usafi ya Ng'arisha Nzengo Uchafu Nuksi.

Burudani ilikuwa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza kisha itahamia kwenye minada yote Jijini Mwanza ambapo kulikuwa na makumi ya wasanii walioshusha burudani kali balaa.

Kupitia burudani, Lake Fm inahamasisha suala la usafi minadani na mkoani Mwanza kwa ujumla. Pia kila mnada atakuwa akitafutwa Mama Lishe Bora, Balozi Imara na Mwananzengo Hodari na wote kujipatia zawadi nono.

Burudani za Gulio la Mtaa zimepewa nguvu na Pepsi, Tigo, Busy Bee, Barmedas Tv, Genic Studio, Mama Salakika Deco, Lake Zone Tents & Supply, Mamba Entertainment, CF Hospital, Gerusalem Sound na BMG.
Mkuu wa Vipindi, Lake Fm Mwanza, Yusuph Magupa akiwasilisha shukurani na salamu zake kwa niaba ya wafanyakazi wengine kwenye burudani ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza
Mwenyekiti wa Masoko na Minada, Justine Sagara, akitoa salamu zake kwa Wananzengo
Mkuu wa masoko kutoka Pepsi akitoa salamu zake kwa Wananzengo
Mkuu wa masoko kutoka Tigo akitoa salamu zake kwa Wananzengo
Mkurugenzi wa Lake Fm, Doreen Noni (kushoto) akimpongeza Mama Lishe Bora, Neema Gerald, kutoka mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza na kumkabidhi zawadi yake
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara katika Masoko na Minada mkoani Mwanza, Justine Sagara (kulia), akimpongeza Mama Lishe Bora, Mama Rhobi, kutoka mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza na kumkabidhi zawadi yake
Mkuu wa masoko kutoka Tigo akimpongeza Mama Lishe Bora, Mariam Magembe-Mama Rhobi, kutoka mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza na kumkabidhi zawadi yake
Mkurugenzi wa Lake Fm, Doreen Noni (kulia) akimpongeza mshindi wa nafasi ya MWANANZENGO HODARI, Khatibu Ramadhan ambaye atakuwa balozi wa Lake Fm katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza
Mama Lishe kutoka mnada wa Nyakato National walipata zawadi kutoka Lake Fm
Mtangazaji wa Lake Fm Mwanza, OG akihost show ya Gulio la Mtaa kwenye mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza
Wazee wa burudani, Nshimba ya Nzengo (Simba wa Mtaani) kutoka Jijini Mwanza wakishusha burudani kali
King Silver akishusha burudani burudani ya nguvu kwenye show ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza iliyoandaliwa na Lake Fm Mwanza kupitia kampeni yake ya Ng'arisha Nzengo, Uchafu Nuksi
Mwanamuziki wa Hip Hop Jijini Mwanza, Dogo D akishusha burudani kali kwenye show ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza iliyoandaliwa na Lake Fm Mwanza kupitia kampeni yake ya Ng'arisha Nzengo, Uchafu Nuksi
Wananzengo wakiburudika na show kutoka kwa mwanamuziki Abuu Mkali
Mwanamuziki Abuu Mkali kutoka Jijini Mwanza akiwaburudisha Wananzengo kwenye Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National
Burudani ilikuwa poa sana
Wananzengo Jijini Mwanza wakifuatilia burudani ya Gulio la Mtaa kwenye mnada wa Nyakato National
Wananzengo Jijini Mwanza wakifuatilia burudani ya Gulio la Mtaa
Wananzengo kutoka Lake Fm
Wananzengo kutoka Lake Fm
Wazee wa burudani, Nshimba ya Nzengo (Simba wa Mtaani) kutoka Jijini Mwanza
Wananzengo kutoka Lake Fm Mwanza
Mwananzengo Eve kutoka Lake Fm Mwanza
Mwananzengo kutoka Lake Fm Mwanza
Washirika wetu wa usalama kwenye ubora wao
Washirika wetu wa usalama kwenye ubora wao
Washirika wetu Pepsi wakiendelea kutoa huduma ya vinywaji kwa Wananzengo
Wananzengo wakifuatilia burudani ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza huku Tigo wakiendelea kutoa huduma za kimawasiliano
Kikosi kazi cha kusaka wanyange kutoka Fox Models
Akina mama lishe wa mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Lake Fm
Kikosi kazi cha kuchukua kumbukumbu kwa njia ya picha nyongevu na mnato.

No comments:

Powered by Blogger.