LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA MKOANI TANGA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha  Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako Tanga.
Mwijage ameyafungua maonyesho hayo leo katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha  Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa jana Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.
 Waziri wa viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa  pamoja na mafuta aina mbalimbali.
 Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho Tanga
Wakazi wa Tanga wakiangalia Kobe ambaye ni moja ya vivutio katika maonyesho ya tano ya Kimataifa yanayofanyika Tanga. 
TangaKumekuchaBlog

No comments:

Powered by Blogger.