LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WAADHIMISHA SIKU YA HEDHI DUNIANI 2017.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 #BMGHabari
Tanzania leo jumapili Mei 28, 2017 inaungana na mataifa mengine kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Heshi duniani.

Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Dodoma ambapo kimkoa Mwanza yanafanyika kwenye Uwanja wa mpira Nyamagana.

Shughuli ya maadhimisho hayo mkoani Mwanza imeatibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Youth With New Hope in Life Organization (TAYONEHO) la Jijini Mwanza, kwa ushirikiano wa karibu na Shirika la kimataifa la Plan International, Mwanza.

"Matembezi yanaanzia ukumbi wa Ghandhi Hall asubuhi yakiwahusisha vijana wa kike na kiume pamoja na wanaume na wanawake na yatapokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, katika uwanja wa Nyamagana". Amebainisha Mkurugenzi wa Shirika la TAYONEYO, Dkt.Iman Tinda.

Lengo la maadhimisho hayo ni kuvunja ukimya juu ya masuala ya hedhi ikiwemo kuondokana na dhana potofu kwamba hedhi ni ugonjwa pamoja na namna bora ya kuhakikisha mtoto wa kike anajiweka katika hali ya usafi ili abaki shuleni badala ya kukosa masoko kila apatapo hedhi. 

Siku ya hedhi duniani ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014 baada ya kuidhinishwa Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo ni mara ya kwanza kuadhimishwa mwaka huu 2017 nchini Tanzania.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Hedhi duniani 2017 ni "Elimu juu ya Hedhi hubadili kila kitu".

No comments:

Powered by Blogger.