LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAMADHANI CUP YAPAMBA MOTO JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand,Mwanza
Wadau na wapenda michezo mkoani  hapa, wametakiwa kushiriki katika mashindano ya ligi ya  Ramadhani Cup  yaliyoshirikisha timu12 kutoka katika wilaya ya  Ilemela na Nyamagana, ambayo yameanza kutimua vumbi hivi karibuni katika  uwanja wa Mirongo   jijini  Mwanza.

Akizungumza jana na BMG  Mkurugenzi wa Ramadhani Cup Shafii Said (Chaku),alisema lengo   la mashindano hayo ni kuwaepusha vijana katika makundi mabaya hasa katika kipindi hiki cha  mwezi  Mtukufu wa Ramadhani pamoja na  kukuza na kuendeleza vipaji.

Chaku alisema  katika  msimu  huu wanatarajia kuwepo na upinzani mkubwa kulinganisha na misimu iliyopita kwa sababu timu shiriki zitakuwa na wachezaji tofauti hasa wengi wakitokea ligi kuu kwa kuwa wapo Mwanza kwa ajili ya mapumziko. 

 Pia alisema timu ambazo tayari zimekwisha jisajiri kushiriki katika mashindano hayo  ni  Marsh Athlestics, Rumumba Mirror Clane, Uhuru Rangers, Baiko, anaendelea kukamilisha ushiriki wa timu nyingine.

 “Mwezi wa Ramadani   ni kipindi cha toba nimeandaa mashindano haya, ili kuwasaidia  vijana kujiepusha na makundi mabaya ambayo yanaweza kuchoche kufanya dhambi kitu ambacho hakifai kwa kipindi hiki ambapo mpaka sasa ni msimu wa tisa tangu kuanzishwa kwake,"alisema Chaku.

Hata hivyo alisema zawadi ambazo zitatolewa kwa washindi ni mbuzi wawili na kombe kwa mshindi wa kwanza, na mbuzi mmoja kwa mshindi wa pili na zitakuwa na thamani ya sh.950000, amechagua zawadi hizo akiwa na  lengo za kutumika kama kitoweo katika siku ya sikukuu ya Eid.

No comments:

Powered by Blogger.