LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATOTO KUTOKA COMPASSION KUCHUANA VIKALI JIJINI MWANZA

BMG Habari, Pamoja Daima!

Fainali ya mashindano ya watoto kutoka Vituo vya Huduma ya Mtoto (Compassion) Kanda ya Mwanza, inatarajiwa kufanyika kesho jumamosi Agosti 26,2017 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi, Joram Samwel amesema mashindano hayo yalianza tangu Mei 25 mwaka huu kwa kuhusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete pamoja na riadha.

Amesema timu ya soka ya watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 ya Anglikana Igoma itachuana na wenzao kutoka Moravian Kigoto kwenye mchezo wa fainali huku timu ya watoto wenye umri kama huo kutoka AIC Bujora ikichuana na wenzao timu ya PAG Mabatini ili kumsaka mshindi wa tatu.

Upande wa timu ya soka ya watoto wenye umri kati ya miaka minane hadi 12 ya EAGT Buzuruga itacheza wenzao kutoka AIC Buhongwa kwenye mchezo wa fainali huku.

Katika fainali ya mchezo wa mpira wa pete, timu ya watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 ya Anglikana Igoma,itacheza na wenzao kutoka TAG Nyakato huku wale wenye kati ya miaka minane hadi 12 kutoka FPCT Pasiansi wakicheza na wenzao kutoka Moravian Kigoto.

Joram Samwel amesema lengo la michuano hiyo ni kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto ambapo wamewasihi wazazi, walezi, watoto pamoja na wapenzi wa michezo Jijini Mwanza, kujitokeza kwa wingi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi ili kushuhudia fainali hiyo ambayo itakuwa na mvuto wa kipekee.
Tazama video hapo chini

No comments:

Powered by Blogger.