LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC MTATURU ASHINDA UJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akionyesha namba yake ya ushiriki ambayo ni namba 6 mara baada ya kuzungumza mbele ya wajumbe kuwaomba kura
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitumia haki yake ya kikatiba ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya CCM

Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wakifatilia mkutano huo uliomalizika kwa salama na amani

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa kwa kishindo. katika nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo Ndg Hassan Tati wakifatilia mkutano Mkuu wa CCM
Na Mathias canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Leo Jumamosi Octoba 7, 2017 amewazidi mbinu za ushawishi washindani wenzake 10 waliokuwa wakiwania nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.

Wajumbe 989 kati ya wajumbe halali waliojiandikisha 1034 wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wamemuwezesha Mhe Mtaturu kuwa kinara katika matokeo hayo kwa kuungwa mkono kwa kura nyingi.

Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa kauli moja wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi  eneo na Kata ya Ikungi na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

Mjumbe huyo wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Mhe Mtaturu ataungana na wenzake walioshika nafasi ya pili na ya tatu ambao ni Mwanga Ally Juma aliyepata kura 620, na Yunde Celestine Kimu aliyepata kura 612 kuwakilisha Wilaya ya Ikungi katika kikao muhimu cha maamuzi cha CCM Taifa.

Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Mhe Mtaturu amesifu imani kubwa aliyoonyeshwa na wajumbe wote huku akiwasihi kuonyesha zaidi ushirikiano katika kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.

Aliahidi kutekeleza na kusimamia kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 huku akiwasihi wananchi kwa kauli moja kushirikiana na Viongozi wote wa Chama na serikali hususani kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia wananchi pasina kujali maslahi yake binafsi. 

Mhe Mtaturu aliwasihi wajumbe wote kuwaunga mkono washindi wa nafasi zote za uongozi ndani ya CCM ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika kuwatumikia.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha uchaguzi wa ngazi ya chama na hata serikali kila mwananchi huwa na maono na mtazamo wake kwa kiongozi amtakaye lakini pindi anapochaguliwa kiongozi mmoja ni wazi ni vyema ikawa mwisho wa makundi hayo hivyo kuwa na mshikamano mpya katika uwajibikaji.

Wagombea wengine ambao hawajafanikiwa kuvuka kiunzi katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ni pamoja na Ayubu Heleni Petro, Bollosi Tatu Mohamed, Mghenyi John Mathias, Mghenyi Juma Shabani, Mkhotya Prorice Patrick, Muna abubakar Omary, Siphy Iddy Selemani, na Sunja Mussa Ntandu.

No comments:

Powered by Blogger.