LIVE STREAM ADS

Header Ads

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAWAJENGEA UWEZO MADAKTARI KANDA YA ZIWA

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na Binagi Media Group
Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF umetoa semina kwa Waganga na Madkatari Kanda ya Ziwa ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathimini sahihi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini kwa ajili ya kulipwa fidia.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba amesema ujio wa mfuko huo ni faraja kwa waajiri na waajiwa kwani umelenga kuondoa kero walizokuwa wakizipata wafanyakazi baada ya kuumia kazini hivyo semina hiyo itasaidia madaktari hao kufanya tathmini za malipo kwa haraka zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa semina hiyo, amewasihi waajiri wote kujiunga na mfuko huo na kwamba ni kosa kisheria kwa waajiri wanaokwepa kujiunga na kutoa michango kwa ajili ya waajiriwa wao.

Dkt.Furaha Munema kutoka hospitali ya Rufaa mkoani Mwanza Sekou Toure ambaye ni mmoja wa madaktari walionufaika na semina hiyo ya siku tano kuanzia leo, amebainisha kwamba itawasaidia kutenda haki wakati wa tathmini kwa mfanyakazi atakayekuwa ameumia kazini.

Naye mmoja wa wawezeshaji wa semina hiyo Dkt.Robert Mhina ambaye ni daktari bingwa upasuaji mifupa kutoka hospitali ya taifa Muhimbili kitengo cha mifupa MOI, amesema mfuko wa fidia WCF umesaidia kuondoa usumbufu uliokuwepo hapo awali baada ya wafanyakazi kuumia kazini.


Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF unatoa huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, msaada wa mazishi, malipo kwa wategemezi ikiwa mfanyakazi atafariki dunia, ukarabati pamoja na ushauri nasaha.
Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati), akiwa pamoja na viongozi wa WCF.
Baadhi ya Waganga na Madaktari wanaoshgiriki semina hiyo katika ukumbi wa Kenki Kuu BOT Jijini Mwanza.
Picha zaidi bonyeza Binagi Media Group

No comments:

Powered by Blogger.