LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko akutana na wazalishaji wa chumvi na jasi mikoa ya Lindi na Mtwara

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko akizungumza na wazalishaji wa chumvi, wachimbaji wa jasi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na uongozi wa kampuni ya Dangote, jana Julai 21, 2018 Mjini Mtwara.
 Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko amekutana na wazalishaji wa chumvi, wachimbaji wa jasi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na uongozi wa kampuni ya Dangote na kuwahimiza kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria ya madini ikiwemo kulipa kodi sahihi.

Ni katika kikao kilichofanyika jana katika Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini iliyopo mkoani Mtwara ambapo aliwahimiza wazalishaji chumvi kuongeza uzalisha zaidi ili kukidhi mahitaji ya taifa badala ya kutegemea chumvi kutoka nje ya nchi.

Alisema Tanzania ina fursa kubwa ya biashara ya chumvi ambapo mahitaji kwa mwaka ni zaidi ya tani laki tatu huku uwezo wa ndani wa kuzalisha chumvi ukiwa ni tani 120,000 hivyo wazalishaji watumie vyema fursa hiyo na kuzalisha chumvi kwa wingi ili kukidhi mahitaji ambapo kwa sasa tani zaidi ya laki mbili zinaagizwa nje ya nchi.

Aidha aliwataka wachimbaji wa madini ya jasi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya madini kifungu cha 87 kinachomtaka mfanyabiashara wa madini kulipa mrabaha kwa bei ya kituo cha mwisho cha kuuzia madini (Gross Value) badala ya bei ya mgodini (net back value).

Awali Mwenyekiti Msaidizi Chama cha Wachimbaji Madini mkoani Mtwara (MTWAREMA), Abdallah Ismail aliishukuru serikali kwa kuondoa baadhi ya kodi na tozo zilizokuwa kero kwa wazalishaji chumvi na kwamba wako tayari kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ikiwemo kulipa kodi stahiki.

Akitoa taarifa ya kero za wazalishaji chumvi zilizoshughulikiwa baada ya kikao cha wazalishaji hao na Naibu Waziri Biteko kilichofanyika Januari 19 mwaka huu, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mayigi Makolobela alibainisha baadhi ya tozo zilizoondolewa kuwa ni pamoja na ushuru wa chumvi, ada ya ukaguzi, ada ya jangwa na andiko mradi na hivyo kuwataka kulipa kwa uaminifu tozo na kodi zilizosalia.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mayigi Makolobela
Mwenyekiti Msaidizi Chama cha Wachimbaji Madini mkoani Mtwara (MTWAREMA), Abdallah Ismail
Naibu Waziri Mhe.Doto Biteko akisisitiza wachimbaji wa madini nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ikiwemo kulipa kodi stahiki
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Chumvi mkoani Mwatra (MTWAREMA), Festal Balegele (kulia) aliomba serikali kuwawezesha wazalishaji chumvi kwenda nchini Kenya kujifunza namna ya uzalishaji chumvi yenye ubora
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali ikiwemo ofisi ya madini
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko (kushoto) pia alikutana na Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe.Gelastus Byakanwa (kulia).

No comments:

Powered by Blogger.