LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri Doto Biteko akemea vitendo vya rushwa sekta ya madini

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko amefanya ziara katika machimbo ya Ngapa yaliyopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kuzungumza na wachimbaji wadogo wanaochimba madini ya vito aina ya "Gem Stone" katika machimbo hayo. Naibu Waziri Biteko alifanya ziara hiyo Julai Julai 19, 2018 katika machimbo hayo na kutumia fursa hiyo kuwatahadharisha maafisa madini nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa migodini badala ya kuwasaidia wachimbaji hususani wachimbaji wadogo ili wafanye shughuli zao vyema.​
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri Doto Biteko akiangalia namna uoshaji wa madini ya vito unavyofanyika alipotembelea machimbo ya Ngapa
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo katika machimbo ya Ngapa wilayani Tunduru
Wachimbaji wadogo wa Ngapa wakimsikiliza Mhe.Biteko
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe.Juma Homera akizungumza kwenye mkutano huo na kuahidi serikali kuendelea kuwafikishia huduma muhimu ikiwemo mawasiliano ya simu pamoja na barabara wachimbaji wadogo wa machimbo ya Ngapa
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wilayani Tunduru.
Naibu Waziri Mhe.Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wilayani Tunduru na wachimbaji wadogo wilayani Tunduru.

No comments:

Powered by Blogger.