LIVE STREAM ADS

Header Ads

FURSA: Aina 13 za madini zinazopatikana Gairo mkoani Morogoro

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro ni miongoni mwa wilaya zilizobarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini hapa nchini hivyo wawekezaji wanahimizwa kuchangamkia fursa hiyo. Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Siriel Mchembe anasema bado serikali haijaanza kunufaika vya kutosha kutokana na madini hayo na hivyo kuomba Wizara ya Madini kuweka mikakati bora ya kuhakikisha madini hayo yanaleta tija kwa wananchi na serikali kwa ujumla. Hayo yanabainishwa kwenye ziara ya siku moja ya Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko aliyoifanya wilayani Gairo Julai 11, 2018 na kutembelea machimbo mbalimbali ya madini ikiwemo machimbo ya Rubeho na baadae kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Rubeho, Jumba Dimwe pamoja na Kichangani. PIA SOMAAkamatwa na madini nyumbani kwake

No comments:

Powered by Blogger.