LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri wa Afya afanya ziara Hospitali ya Sekou Tour Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, BMG
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt. Faustine Ndungilile amewataka wananchi kukemea na kuacha kufanya vitendo vya  ukatili  wa jinsia hasa kwa wanawake na watoto.

Dkt.Ndugulile alitoa wito huo jana alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure na kubainisha kwamba serikali katika kuhakiksha inakomesha  vitendo vya ukatili imeanzisha  vituo vya pamoja katika hospitali  za mikoa nchini kikiwemo cha Mwanza ambacho kinaitwa “One Stop  Centre” lengo ikiwa ni wahanga wa vitendo vya ukatili kupata huduma kwa pamoja ikiwemo za dawati la jinsia la polisi, ushauri na nasaha pamoja na matibabu.

Alisema asilimia kubwa ya  vitendo vya ukatili hufanywa na watu wa karibu ikilinganishwa na uhalifu mwingine hivyo ni jukumu la jamii kukemea na kuacha kufanya vitendo hivyo.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dkt. Bahati Msaki alisema kituo hicho cha “One Stop Centre” kinatoa huduma kwa wahanga waliofanyiwa    ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo wa kijinsia, kiuchumi, kimwili na  kingono.

Dkt.Bahati Msaki alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni watu kutokuwa na uelewa wa  kuwahi hospitalini ndani ya masaa 72 endapo wamefanyiwa ukatili wa kingono ili kupata dawa za kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi VVU na mimba huku pia asilimia kubwa wakishindwa kutambua viashiria vya ukatili wa kijinsia.

No comments:

Powered by Blogger.