Wakulima kupata pembejeo za kilimo kwa wakati
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LIMITED Peter Kumalilwa akieleza mipango mbalimbali ya kampuni hiyo katika kumkwamua mkulima wa Tanzania.
Na William Bundala
Kampuni ya
usambazaji ya Pembejeo ya PETROBENA EAST AFRICA LTD imeanza kuunga mkono kwa
vitendo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungwano wa Tanzania Mh John Pombe
Magufuli kwa kuhakikisha wanafikisha pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima
nchini.
Akiongea mkoani Morogoro katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa
maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA
Peter Kumalilwa amesema wameamua kuweka Ghala kubwa mkoani Morogoro ili
kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka
kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.
Kumalilwa
alisema PETROBENA ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya YARA watahakikisha
mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika
maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali
inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa
walipo wahitaji.
Aliongeza
kuwa katika mkoa wa Morogoro wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao
700 katika wilaya zote sita ambao watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo
itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo
wa Miwa,Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.
Naye Afisa
Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini, John Meshak alisema wameamua
kuzindua ghala la mbolea Morogoro kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao
mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza
kasi ya uzalishaji wa mazao yao.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Wakulima wa Miwa wilaya ya Kilombero Bakari Mkangamo
akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake aliipongeza kampuni ya PETROBENA ambao
ni wakala mkuu wa YARA kwa kuwafikishia pembeo kwa wakati,na kuongeza kuwa
kuanzia msimu ujao uzalishaji utaongezeka kwa kuwa wakulima wamelima na kuwekea
mbolea kwa wakati tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Mwishoni mwa
mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
alitoa wito kuhakikisha kwamba Mbolea na pembejeo zingine zinapatikana muda
wote zinapohitajika tena na kwa gharama nafuu ambapo Kampuni ya PETROBENA EAST
AFRICA LTD ambao ni wakala wakuu wa Kampuni ya Mbolea ya YARA wameanza
kutekeleza agizo hilo kwa mikoa ya Dar es salaam,Tabora,Morogoro,Njombe na
Arusha.
Mtaalamu wa kilimo kutoka kampuni ya YARA Maulid Mkima
akitoa darasa la kwa maafisa kilimo na maafisa wa pembejeo katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi mpya ya PETROBENA mkoani Morogoro.
Afisa biashara wa kampuni ya YARA Nyanda za Juu Kusini John
Meshack akiongea na Maafisa Milimo pamoja na Wauzaji wa Pembejeo
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA
LIMITED Peter Kumalilwa akisikiliza kwa makini darasa lililokuwa likitolewa na
Mtaalamu wa Kilimo kutoka kampuni ya YARA bwana Maulid Mtima.
Maafisa Kilimo na Wauzaji wa Pembejeo kutoka wilaya za mkoa
wa Morogoro wakiwa makini katika mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo na
umuhimu wa kutumia mbolea.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka Kampuni ya PETROBENA
Sabena Kubini aliyesimama kulia amevaa t-shirt nyeupe pamoja na maafisa wengine
wa PETROBENA na YARA wakisikiliza elimu ya matumizi bora ya mbolea kutoka kwa
mtaalamu wa kilimo wa kampuni ya YARA hayupo pichani.
Maafisa kilimo na wauzaji wa pembejeo wakiwa makini
kusikiliza mafunzo kuhusu umuhimu wa matumizi bora ya mbolea na madhara ya
kutumia mbolea tofauti na maelekezo ya wataalamu.
Maafisa kilimo,wauzaji wa pembejeo na wafanyakazi wa kampuni
ya PETROBENA wakiwa darasani wakiendelea kupata mafunzo ya matumizi bora ya
mbolea katika ukumbi wa mikutano wa ofisi mpya za PETROBENA zilizopo Nane nane
mkoani Morogoro.
Mafunzo yakiendelea
No comments: