Jeshi la zimamoto mkoani Mwanza latahadharisha ujenzi wa makazi holela
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza limewatahadharisha
wananchi kujiepusha na ujenzi wa makazi katika maeneo hatarishi ikiwemo kwenye
miinuko mikali kutokana na usalama mdogo wa maeneo hayo hususani wakati wa
majanga.
Kamishina
Msaidizi wa Jeshi hilo, Juma Kwiyamba
anasema changamoto zinazowakabili katika utendaji wa kazi ni baadhi ya maeneo
kutofikika kirahisi pindi wanapotaka kutoa huduma ya kuzima moto na uokoaji wa
watu na mali zao kwani miundombinu yake
siyo rafiki kutokana na ujenzi holela ulifanya na wakazi wa eneo husika hususani milimani.
Sanjari na
hayo alisema, ujenzi holela umesababisha uharibifu wa miindombinu ya maji kwa
kuziba au kufukia visima maalum vya maji ya kuzimia moto (fire hydrants), hivyo
kupelekea upatikanaji maji kuwa mgumu
wakati wa zoezi la kuzima moto na kuokoa
mali na watu sanjari na baadhi ya madereva wa magari yanayotoa huduma tofauti
kwa jamii kushindwa kuwapisha barabarani
pindi wanapoku wanaenda kutoa msaada eneo
ilipotokea dharura ya moto matokeo yake wanaweza kusababisha ajali.
Aidha aliwataka
wananchi kukata bima za nyumba, hoteli, majengo marefu na vifaa vya moto kama
magari ya aina mbalimbali, pikipiki na bajaji ili ajali ya moto inapotokea wawe wamekidhi vigezo
vinavyoitajika na kampuni ya bima husika
ili waweze kupatiwa stahiki zao zinazowahusu pamoja na kuzingatia
tahadhari ya moto na kukubaliana na ukaguzi unaofanywa na jeshi hilo.
Alisema jeshi
hilo linafanya ukaguzi kwa lengo la
kuboresha na kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwenye maeneo husika,
kubaini vihatarishi vya moto, kutoa mbinu za kuzuia majanga pamoja na kukabiliana na moto katika hatua za awali.
"Ni
zoezi linalolenga kutoa ushauri wa kitaalum na kisheria kwa umma pamoja na
kuweka miundombinu ya tahadhari sanjari na kinga ya kuzuia, kupambana na
kuwawezesha watumiaji kujiokoa kirahisi wakati wa dharura", alisema
Kwiyamba.
Tamasha la Kinga na Tahadhari dhidi ya Majanga na Moto Jijini Mwanza
No comments: