LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Mwanza afanya mazungumzo na Kamanda mpya wa jeshi la Polisi

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) leo amekutana na kufanya mazungumzo mafuki na Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoani hapa, ACP. Jonathana Shanna (kulia) aliyefika ofisini kwake kujitambulisha.

Pia Mhe. Mongella ametumia fursa hiyo kuagana na aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoani Mwanza DCP. Ahmed Msangi (kushoto) ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam ambapo mazungumzo yao yamejikita katika kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza.

Mapema asubuhi ACP. Shanna akizungumza na maafisa wa jeshi la polisi mkoani Mwanza, alionya kuhusu vitendo vya uhalifu na kuahidi kuvitokomeza ambapo DCP. Msangi aliwasihi maafisa hao kumpa ushirikiano wa kutoka kama waliokuwa wakimpa ili kutimiza vyema majukumu yake.

No comments:

Powered by Blogger.