LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanahabari Mathias Canal auaga ukapera

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Mwandishi Mathias Canal akivishwa Pete na mkewe Bi Elizabeth Chagamba wakati wa ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
Maharusi wakionyesha cheti cha ndoa
Bwana harusi Mathias Canal na Bi harusi Elizabeth Chagamba wakicheza wimbo maalumu ulioimbwa na msanii wa midondoko ya (RnB) Elias Barnabas maarufu Barnaba Boy Classic wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi
Mwandishi Mathias Canal akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji J. Mtaturu wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi
Mwandishi Mathias Canal na mkewe Bi Elizabeth Chagamba (walioketi) pamoja na watumishi wa Wizara ya Kilimo wakiongozwa na waziri wa wizara hiyo Mhe Dkt Charles Tizeba, Watumishi kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakati wa hafla ya jioni.

Na Wazo Huru Blog
Mwandishi na mchambuzi wa Habari nchini Tanzania ambaye ni Afisa Habari Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA)-Wizara ya kilimo ameingia kwenye historia ya vijana wachache waliofanya maamuzi ya busara na tija katika mustakabali wa maisha mema katika jamii kwa kufunga ndoa Takatifu.

Ibada ya ndoa Takatifu ilifanyika siku ya jumamosi tarehe 18 Agosti 2018 kuanzia majira ya saa sita na nusu (6:30) mchana mpaka saa nane na nusu (8:30) mchana katika kanisa la Kiinjili La Kilutheli Tanzania-Usharika wa Mabibo Farasi Jijini Dar as salaam.

Mathias Canal amefunga ndoa na Binti mstaarabu, wenye nidhamu na busara huku akiwa mcha Mungu Bi Elizabeth Chagamba mzaliwa wa Tanga ambaye kihistoria tangu kufahamiana urafiki wao umedumu kwa takribani miaka sita mpaka kufikia maamuzi ya kufunga ndoa Takatifu.

Ibada hiyo ya ndoa Takatifu iliendeshwa na Mchungaji Remmya Chuma kutoka kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Mashariki ya Pwani Usharika wa Kawe Jijini Dar es salaam ambapo aliwataka Bwana Harusi Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kuishi kwa kuzingatia misingi ya ndoa na agano Takatifu baina yao na Mungu kwani ndoa yao imeshuhudiwa na watu duniani lakini shahidi pekee mwenye maono zaidi ya ndoa hiyo ni Mungu mwenyewe.

Mchungaji Chuma aliwakumbusha waumini wengine katika ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kila hatua wanazopita huku akiwasihi waumini hususani vijana ambao hawajafunga ndoa Takatifu kuingia katika tendo hilo muhimu machoni pa wanadamu na Mungu wa Mbinguni. Na kuongeza kwa kunukuu Kitabu cha Mathayo 19:5 kisemacho, "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha Baba na Mama yake ataambatana na Mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja".

Mara baada ya Ndoa Takatifu kati ya Afisa Habari NFRA Ndg Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kukamilika kanisani ilihudhuriwa na tafrija fupi iliyofanyika katika eneo la Urafiki Social Hall katika ukumbi wa Nyangumi ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya wananchi huku viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wakihudhuria.

Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi ndoa hiyo ilihudhuriwa na Timu ya uenezi kutoka Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mohammed Alliyan Kaimu Katibu wa Idara ya oganaizesheni na uhusiano wa kimataifa Umoja wa Vijana (UVCCM) Makao makuu pamoja na wasaidizi wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu UVCCM Taifa.

Kwa upande wa serikali hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ambaye katika salamu alizozitoa kwa niaba ya Wizara yake alisema kuwa Ndoa ni muunganiko wa kiagano wa kudumu kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja wenye kuishi na kuwa mume na mke. Neno agano ni neno muhimu sana kwa sababu agano ni patano la milele ambaye shahidi yake ni Mungu mwenyewe wala si mwanadamu hivyo kuwataka sana ndoa hao kuwa waaminifu milele.

Aidha, alitaja umahiri katika utendaji unaofanywa na wasaidizi wake akiwemo Mathias Canal pamoja na mwenzake Innocent Masaka kuwa ni wadogo sana kwake kiumri lakini wamekuwa msaada mkubwa katika kutekeleza majukumu ya serikali yakiwemo na yale ya Chama cha Mapinduzi.

Katika hafla hiyo Mhe Dkt Tizeba alisema kuwa Fungate ni jambo muhimu baada ya ndoa Takatifu hivyo akatoa ofa maalumu kwa maharusi hao kwenda mapumzikoni Mjini Unguja-Zanzibar huku akisema kuwa gharama zote za siku tano atagharamia yeye. Pia Dkt Tizeba ametoa ofa ya mapumziko ya siku tano kwa Ndg Mathias Canal ambaye muda wake wa mapumziko ulikuwa umemalizika hivyo kuendelea na mapumziko ya siku tano.

Tayari Mathias Canal na Mkewe Bi Elizabeth Chagamba wamewasili Mjini Unguja-Zanzibar ambapo katika mapumziko hayo wamesafiri na wapambe 10 waliohudumu katika sherehe yao (Maids) ili kufurahi kwa pamoja katika mapumziko hayo.

No comments:

Powered by Blogger.