Tambo za Alliance na Mbao kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Ligi Kuu ya
soka Tanzania Bara msimu wa mwaka 2018/19 unaanza rasmi kutimua vumbi hii leo
Agosti 22, 2018 ambapo kwa Jiji la Mwanza mashabiki wanatarajia kushuhudia soka
la ushindani baina ya timu za Alliance FC na Mbao FC katika uwanja wa CCM.
Kocha wa timu
ya Alliance FC, Mbwana Makata anasema maandalizi yanaendelea vyema na kikosi
chake kimejipanga kuhakikisha kinaibuka na ushindi kwenye mchezo huo licha ya
kwamba ni mara yao ya kwanza kushiriki ligi hiyo.
"Matumaini
ya kupata ushindi ni makubwa katika mechi ya ufunguzi dhidi ya majirani zetu
Mbao FC kwani tumejiandaa kwa kucheza michezo mingi ya kirafiki na timu ambazo
zina uzoefu katika ligi kuu ikiwemo Kagera Sugar, Singida United, Stend United
na Biashara FC hivyo zimetufanya tujiamini" Alisema Makata.
Alisema
wachezaji wake wawili Jamal Sudi na Juhudi Samweli wataukosa mchezo huo wa
ufunguzi kutokana na kushtuka nyama za paja licha ya kwamba hali zao
zinaendelea vizuri japo bado wapo katika matibabu.
Nahodha
wa Alliance FC, Hance Masoud alisema wamejiandaa vyema na wachezaji wana morali
ya kufanya vizuri hivyo mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi
kuishangilia timu yao kwenye michezo yote.
Naye Kocha
wa Mbao FC, Amri Said alisema anajivunia timu timu hiyo na anamatumaini makubwa
ya kufanya vizuri katika mchezo huo na ligi kwa ujumla na kwamba kikosi kipo
kamili kwani wamecheza mechi nyingi za
kirafiki kwa ajili ya kujiandaa.
Aliwapongeza
mashabiki kwa mshikamano waliouonyesha msimu uliopita hivyo aliwaomba kuendelea
kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika msimu.
No comments: