Wakazi wa Kanda ya Ziwa sasa kujishindia Mamilioni na Pepsi
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Kampuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji
na wasambazaji wa vinywaji baridi aina ya Pepsi, Mirinda, 7up, Mountain Dew na
Evervess, Mkoani Mwanza wanayo furaha kuwaletea Shindano kabambe litakalojulikana kwa jina la“Jishindie
Mamilioni ” Shindano hili litahusu
soda aina ya Pepsi, Mirinda Orange, Mirinda Fruity, Mirinda Lemon, 7Up
za ujazo wa mililita 350, na Mountain Dew (300ml).
Shindano hili
litatangazwa Katika Radio, Magazeti, Mabango na Vipeperushi mbalimbali. Madhumuni
ya kuwaletea shindano hili niKuboresha hali ya maisha ya wateja wetu wa kanda
ya Ziwa kwa kuwapatia zawadi za fedha taslimu ili kuwawezesha kujikomboa
kiuchumi.
Shindano hili litaendeshwa Kwa muda wa wiki sita kuanzia tarehe
01/08/18 hadi 16/09/18 katika mikoa ifuatayo: Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Tabora, Geita,
Kigoma na Kagera.
Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja akionesha moja ya mabango ya kutambulisha shindano la Jishindie Mamilioni.
Kutoka kushoto ni Phocas lusato Meneja Rasilimali watu SBC, akifuatia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Hussein Mkwawa ambaye ni Meneja mauzo Kanda ya Ziwa wakisikiliza vyema maswali ya waandishi wa habari (hawako pichani) katika utambulisho rasmi wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
"Safiiiiii.....!!"
Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kulia) akitoa maelezo kwa wawezeshaji SBC, anayemsikiliza mbele yake ni Meneja Mauzo kanda ya Ziwa Hussein Mkwawa, Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Meneja Rasilimali Watu Phocas Lusato katika utambulisho wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
"Hizi ndizo zawadi"
Nikama wakisemezana "Hebu tuone umepata nini ndani ya kizibo chako...." Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kushoto) Sara Onesmo kutoka Clouds Tv na Johari Shani wa Mwananchi Communication.
Ili Mteja ajishindie zawadi anatakiwa kununua soda za
Jamii ya Pepsi kisha abandue ganda Ndani
ya Kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-, 500,000/-,
10,000/-, 5,000/- 1000/- au Free Pepsi (SODA YA BURE), atakua amejishindia zawadi
hiyo papo hapo.
Zawadi za shilingi 10,000/=, 5000/=,1000/=na Soda ya bure
zitapatikana hapo hapo kwa aliyekuuzia soda, Gari ya Mauzo au Muuzaji wa Jumla.
Vizibo vya zawadi vimeandikwa kwa rangi ya dhahabu, Zawadi za shilingi 1,000,000/-,
500,000/- zitatolewa kiwandani Mwanza tu, Barabara ya Musoma, Nyakato, Kuanzia
saa 4 asubuhi hadi saa 9 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa (isipokua siku za sikukuu).
Hii ndio fursa
nzuri kwa wanywaji wa soda zetu kujishindia Mamilioni kila siku kwa kunywa Soda
zetu, Kuna zawadi nyingi sana, kunywa sasa unaweza kuwa wewe ndio mshindi, ili
uboreshe maisha yako.
Tarehe ya mwisho ya kutoa zawadi ni Tarehe
30 Septemba 2018. Tuna imani
utashirikiana nasi kufanikisha shindano
hili na kuboresha maisha yako.
“Jishindie Mamilioni ”
Imeandaliwa na Gsengo Blog/ Tv
Imeandaliwa na Gsengo Blog/ Tv
No comments: