LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kirumba hiyooo fainali ya Angeline Jimbo Cup 2018

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.


Judith Ferdinand, BMG
Timu ya Kata ya Ibungilo na Kirumba imefanikiwa kufuzu kuingia fainali katika mashindano ya Angeline Jimbo Cup msimu wa 2018/19.

Katika fainali hiyo ambayo inachezwa kesho Septemba 17, 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu  Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Walemavu Athony Mavunde.

Kirumba imefuzu kuingia fainali baada ya kuichapa Nyakato goli 1-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa sabasaba kupitia mshambuliaji wake  Baraka David dakika ya 66 huku Ibungilo ikifanikiwa kuilaza chali Kawekamo kwa kufunga goli 1-0 kupitia Tete Jadwa.

Akizungumza na BMG, Kocha wa timu ya Ibungilo Swala Daud alisema, anamshukuru Mungu hadi kufikia fainali na  Chapili ni Mbunge Angelina Mabula kwa kuanda michuano hiyo pamoja na  mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano walioonesha.

Pia alisema mchezo wa   fainali  ni mgumu lakini wao  wamejianda kushinda kwani wanaamini  Kirumba  watakuwa na lengo la kulipiza kisasi baada ya  kuwafunga katika mechi ya ufunguzi.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atajinyakulia  kitita cha milioni 2, kombe, mpira mmoja pamoja na seti moja ya jezi, mshindi wa pili ataondoka na  milioni 1.5, kombe,  jezi seti moja na mpira mmoja huku wa tatu akipata milioni 1, kombe, mpira pamoja na jezi seti moja.

No comments:

Powered by Blogger.