LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Mwanza akabidhi pikipiki kwa Maafisa Elimu

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amekabidhi pikipiki 18 kwa Maafisa Elimu Kata katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), lengo likiwa ni kuchochea ufanisi na utendaji kazi ndani ya Kata zao.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo iliyofanyika leo Septemba 10, 2018 katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mhe. Mongella amewataka Maafisa Elimu hao kuzitunza na kuzitumia vyema kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Pikipiki hizo zimetolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu kupitia program ya EQUIP-T na LANES zikiwa na thamani ya shilingi Milioni 54.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo
Maafisa Elimu Kata na waalimu Jijini Mwanza wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella
Tazama BMG Online Tv hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.