LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yatatua adha ya usafiri kwa Maafisa Elimu Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetoa pikipiki kwa Maafisa Elimu Kata mkoani Mwanza ili kuwaondolea adha ya usafiri na kuongeza ufanisi na utendaji kazi katika Kata zao.

Kwa upande wa Jiji la Mwanza (Nyamagana), Maafisa Elimu katika Kata zote 18 wamekabidhiwa pikipiki zao hii leo Septemba 10, 2018 na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella ambaye amewahimiza kuzitumia vyema ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kurahisisha utendaji kazi wao.

Kaimu Afisa Elimu Jijini Mwanza Philipo Mukama amesema pikipiki hizo zina gharama ya shilingi milioni 54 na kwamba zimetolewa kupitia program ya EQUIP na LANES.
Tazama BMG Online Tv hapa chini

SOMA Mkuu wa Mkoa Mwanza akabidhi pikipiki kwa Maafisa Elimu

No comments:

Powered by Blogger.