LIVE STREAM ADS

Header Ads

GEITA: Biteko akabidhi vyeti kwa washindi wa Maonesho ya Teknolojia ya Dhahabu

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Mwl. Doto Mashaka Biteko amekabidhi makombe, vyeti vya washindi na wadhamini wa maonesho ya kwanza ya teknolojia ya uchimbaji dhahabu yanayofanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.
Mchapalo ukiendela
Mgeni rasmi akikata ndafu kuashilia ufunguzi wa mchapalo huo
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa kampuni ya GGM
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa kampuni ya GGM
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa benki ya Azania
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa benki ya CRDB
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa benki ya NBC
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa kampuni ya Otonde
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa halmashauri ya Geita Vijijini
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akikabidhi cheti kwa kampuni ya bima ya NHIF
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akimkabidhi cheti mkurugenzi wa taasisi ya METDO Tanzania, Ashraf Omary ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Mwl. Doto Biteko akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Chacha Wambura ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Waja General
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Mwl. Doto Mashaka Biteko amekabidhi makombe, vyeti vya washindi na wadhamini wa maonesho ya kwanza ya teknolojia ya uchimbaji dhahabu yanayofanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.

Mhe. Mwl. Biteko alifanya shughuli hiyo jana kwenye mchapalo wa jioni baada ya mapema mchana maonesho hayo kufungwa rasmi na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ingawa alitoa ridhaa ya kuendelea hadi kesho kutwa jumatano kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Robert Gabriel.

Katika hafla hiyo, kampuni ya Anglo Gold Ashanti (GGM) LTD iliibuka mshindi wa jumla ikifuatiwa na benki ya NBC pamoja na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA). Tuzo ya heshima ilichukuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) pamoja na banda maalum la wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Aidha kampuni ya Anglo Gold Ashanti (GGM) LTD iliibuka mshindi kwa kuonesha teknolojia bora ya uchimbaji madini kwa upande wa makampuni makubwa ikifuatiwa na Acacia Bulyanhulu Gold Mine LTD pamoja na Acacia Buzwagi Gold Mine LTD.

Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo Mine iliibuka mshindi upande wa makapuni madogo na ya kati ikifuatiwa na Busolwa Gold Mining LTD pamoja na NGM Gold Mining LTD. Kwa upande wa taasisi za kifedha, benki ya NBC iliibuka mshindi ikifuatiwa na benki ya CRDB pamoja na benki ya Azania.

Taasisi ya NHIF iliibuka mshindi kwa upande wa taasisi za bima za afya ikifuatiwa na NSSF pamoja na AAR huku Wizara ya Madini ikiibuka mshindi wa kwanza upande wa taasisi za serikali ikifuatiwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi VETA pamoja na Mamlaka ya Mapato TRA.

Ushindi wa kwanza kwa upande wa makampuni yanayotoa huduma ulienda kwa kampuni ya Waja General ikifuatiwa na NAPOLI- Kaka Chemicals pamoja na Otonde Group huku Mkoa wa Kagera ukiibuka mshindi upande wa mikoa na halmashauri na kufuatiwa na halmashauri ya Geita Vijijini pamoja na Bukombe. Upande wa wajasiriamali, mshindi wa kwanza alikuwa Anitha Muganda akifuatiwa na Bina Products pamoja na Minzi Manonu.

No comments:

Powered by Blogger.