Naibu Waziri Nyongo akagua migodi ya makaa ya mawe mkoani Songwe
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Meneja Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Alphonce Bikulamchi (katikati) akielezea shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe zinavyofanyika katika Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kabulo uliopo katika mkoa wa Songwe kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto).
Kaimu Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira uliopo katika wilaya ya Ileje Mkoani
Mbeya, Samwel Kibaranga (kushoto)
akimwonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) reli
inayotumika kwa ajili ya kusafirisha makaa ya mawe (haionekani pichani).
Naibu Waziri
wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto mbele) akitoa maelekezo katika
eneo la Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Kiwira.
Naibu Waziri
wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tano kushoto mbele) akiwa katika picha ya
pamoja na wafanyakazi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira mara baada ya
kumalizika kwa mkutano.
Na Greyson Mwase
Tarehe 19
Oktoba, 2018 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alifanya ziara katika
Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kabulo (Kabulo Coal Mine) uliopo katika eneo la
Kabulo lililopo katika wilaya Songwe mkoani Songwe na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa
Kiwira (Kiwira Coal Mine) iliopo katika Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Baada ya
kufanya ziara katika migodi husika, alizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa
Makaa ya Mawe wa Kiwira lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Akizungumza
katika mkutano wa wafanyakazi alisema kuwa, kwa sasa Serikali imetenga fedha
kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya kutoka Kabulo hadi Kiwira itakayotumika
kwa ajili ya usafirishaji wa makaa ya mawe pamoja na kuhakikisha inalipa
stahili za wafanyakazi mara baada ya taratibu kukamilika.
Katika hatua
nyingine, Nyongo aliwataka watumishi kufanya kazi kwa ubunifu na kusisitiza
kuwa Wizara ya Madini itahakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri.
Wafanyakazi
wa Mgodi wa Kiwira walimpongeza Naibu Waziri Nyongo kwa kazi kubwa ya
kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini nchini pamoja na Taasisi
zilizopo chini ya Wizara.
No comments: