Wajasiriamali mkoani Iringa watakiwa kuwa na nidhani ya fedha
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , MNEC Theresia Mtewele aliyeshika Ilani ya Chama cha Mapinduzi akiwa sambamba na diwani wa Kata ya Kitwiru Baraka Kimata, MNEC Mussa Mwakitinya na Mkurugenzi wa TAEDO Kenani Kihongosi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana wa CCM mkoa wa Iringa (UVCCM) akielezea jinsi ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa kutoa elimu mbalimbali ikiwapo elimu ya wajasiliamalia ambayo ilitolewa siku hiyo katika Kata ya Ktwiru kwa wananchi wote waliojitkeza .
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TAEDO, Kenani
Kihongosi ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Iringa, diwani wa Kata ya Kitwiru Baraka Kimata, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele aliyeshika Ilani ya CCM, MNEC Mussa Mwakitinya na diwani wa Kata ya Nduli Bashir Mtove.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Taifa anayewakilisha vijana, MNEC Theresia Mtewele, amewataka
wajasiriamali wa mkoani Iringa kuwa na ubunifu kwenye biashara zao, kuwa na
nidhamu ya matumizi ya fedha za kibiashara ili kukuza mitaji yao pamoja na
kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo itakayowasaidia kujikwamua
kiuchumi.
Akizungumza wakati wa ufunguaji wa
mafunzo ya ujasirilimali yaliyoratibiwa na diwani wa Kata ya Kitwitu, Baraka
Kimata na kutolewa na taasisi ya TAEDO, MNEC Mtewele alisema wajasariliamali
wengi wamekuwa hawakopesheki kwa sababu hawajajiunga katika vikundi.
“Ili kuendana na sera ya serikali ya
viwanda wajasiriliamali hawana budi kujiunga katika vikundi vidogo ili kupata
mikopo itakayowasaidia kuanzisha viwanda vidogo jambo ambalo litawasaidia
kuongeza kipato na ajira kwa watu wengine,” amesema.
MNEC Mtewele aliwataka wajasiriamali
wa Iringa kuwa wabunifu katika biashara zao ili kuweza kufanikiwa zaidi.
“ili mjasiriliamali aweze kufanikiwa
lazima awe na nidhamu na fedha anayopata na si kuitumia hovyo kwani
itasababisha kuyumba kwa biashara na hatimaye kufirisika”.
Kwa upande wake Diwani Kimatha,
alisema aliamua kutoa mafunzo hayo bure kwa wananchi wake ili kujikwamua
kiuchumi na kujijengea ajira kuliko kusubiri kuajiriwa.
Kimata alisema lengo la kufanya hivyo
ni kuwakwamua wananchi wake kiuchumi ikiwa pamoja na kuunga mkono jitihada za
Mh.Rais John Pombe Magufuli juu ya Tanzania ya viwanda huku akiwashauri
viongozi wenzie kutumia nafasi za uongozi kwa kuwasaidia wanaowaongoza.
Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya
Kitwiru mkoani Iringa wamemshukuru diwani wa Kata ya Kitwiru Baraka Kimata kwa
kuwasaidia kupata mafunzo ya
ujasiriamali, huku wakiahidi kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda kwa
kufungua viwanda vidogo vidogo mara
baada ya mafunzo hayo.
No comments: