LIVE STREAM ADS

Header Ads

“Nafuu tukikagua tukute mtu kajinyonga”- RC Geita

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akitoa salamu za shukrani na kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) aliyeanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita jana, kulia ni mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ukarabati na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwanga wilayani Geita.
Wakazi wa Geita walijitokeza kwa wingi kumlaki Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesifia ukarabati na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwanga kilichopo wilayani Geita, na kueleza kwamba serikali itaendelea kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo kuhakikisha hakuna uhaba wa dawa na wataalamu wa afya.

Mhe. Majaliwa aliyasema hayo jana wakati wakiweka jiwe la msingi la ukarabati na ujenzi wa Kituo hicho, kilichopokea shilingi Milioni 500 kupitia mfumo wa “Force Account” na kujenga majengo matano ambayo ni nyumba ya mtumishi (Two in one), maabara, wadi ya akina mama, jengo la upasuaji pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti ambapo bado chenchi ilibaki na kufanya shughuli zingine ikiwemo ujenzi wa njia za wateja kutembea (walking way) na eneo la wagojwa/ wateja kupumzika wakati wakisubiri huduma.

“Tuliwaambia nafuu tukikagua tukute mtu amejinyonga siyo amekula hela ya wananchi”, Alisema Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel wakati akitoa salamu za shukrani.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi mradi mkubwa wa maji wilayani Chato

No comments:

Powered by Blogger.