LIVE STREAM ADS

Header Ads

ACP Abdi Isango awapa somo madereva juu ya usalama barabarani

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Mgeni Rasmi katika wiki ya maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani, ACP Abdi Isango ambaye pia ni Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa (aliyemwakilisha kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani Taifa), akizindua rasmi shughuli hizo za upimaji wa afya kwa madereva wasafirishao mizigo masafa ya mbali iliyoandaliwa na North Star alliance kwa kushirikiana na Puma Energy Foundation, Impala Terminals na Trafigura Foundation.
Henry Mgala Bantu ambaye ni mtaalam wa usafirishaji, uchukuzi, mbobezi wa usalama barabarani, Mjumbe wa Balaza la taifa la usalama barabarani na mwenyekiti wa elimu, mafunzo na uenezi katika baraza hilo, akiwakumbusha madereva mambo mbalimbali muhimu yahusuyo Sheria za barabarani na somo muhimu la madereva kujitambua.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Abben Swai ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania, akiendesha chemshabongo fupi kwa madereva wa magari ya mizigo yaendayo safari ndefu lengo ni kuwakumbusha tu kuendelea kuwa makini pindi wawapo safarini. 
Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Yoronimo Kwesibaga ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Bandari, akitoa salam zake wakati wa wiki ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya barabarani.
Dkt. Sist Agustino Mosha ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Temeke akitoa elimu wa madereva wasafirio safari za mbali kuhusu umuhimu wa kutambua afya zao kipindi chote wawacho safarini, pia kuwakumbusha kutazama afya zao mara kwa mara kabla hawajaanza safari, mwisho aliwakumbusha madereva kuhusina na UKIMWI. 
Mratibu wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama wa Barabarani (RSA) kanda ya Mashariki, David Shao akielezea kwa ufupi umuhimu wa kuwa Balozi wa masuala ya Usalama barabarani na kuwaomba madereva na watu wengine kujumuika kwa pamoja na kuwa mabalozi ili kusaidia kupunguza ajali. 
Mohamed Sharif ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Tanzania na Mkufunzi wa Masomo ya usalama barabarani, akisisitiza kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa kuwa watu mbalimbali wakiwemo askari wa usalama barabarani, madaktari na watu wengine wameungana na madereva ili waje kuwapa elimu na kuwakumbusha mambo muhimu yahusuyo usalama wa barabarani na kujua afya zao maana ni mambo muhimu na yanayoendana kwa ukaribu. 
Mwakilishi kutoka Impala Terminals akitoa salam zake wakati wa mkutano huo, amewashukuru North Star Alliance pamoja na wahusika wa Usalama kwa ajili ya kuhakisha madereva wanasafiri wanapata huduma ya afya kila wawapo safarini na ndio maana katika "yard" mbalimbali hata mikoani kuna ofisi za North Star alliance, aliomba ushirikiano huo uendelee zaidi.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Abben Swai ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania (kulia) akisikiliza majibu ya chemsha bongo kutoka kwa mmoja wa madereva.
Madereva pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika wiki ya kuelekea siku ya Usalama na Afya barabarani katika viwanja vya Impala Terminals.
Mgeni Rasmi katika wiki ya maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani, ACP Abdi Isango ambaye pia ni Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, akijiandaa kuendesha "Scania" ikiwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku hiyo.
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani, ACP Abdi Isango ambaye pia ni Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, akiwa anaendesha "Scania" hilo.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Abben Swai ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania (kushoto) akiwa ndani ya "Scania" kupata maelezo namna ya kuendesha gari hilo kutoka kwa mtaalam wa magari hayo.
Mgeni Rasmi katika wiki ya maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani, ACP Abdi Isango ambaye pia ni Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa akiwa anaungana na madereva wengine kupima afya zao.
Madereva wa Magari ya mizigo yaendayo safari za mbali pamoja na baadhi ya watumishi wa makampuni ya usafirishaji wakipima afya katika mahema ya North Star Alliance.
Picha zote na Fredy Njeje

No comments:

Powered by Blogger.