LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakamatwa Ziwa Victoria kwa tuhuma za uvuvi haramu

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Judith Ferdinand, BMG
Jumla ya wavuvi 21 wakiwemo watanzania na wakenya wamekamatwa wakifanya uvuvi Ziwa Victoria kwa kutumia zana haramu kinyume na katika mwalo wa Bubombi wilayani Rorya mkoani Mara.

Wavuvi hao ambao 15 ni watanzania na sita wakenya walikamatwa Novemba 6, 2018 saa kumi na moja alfajili baada ya doria iliyofanywa na kikosi cha oparesheni sangara mkoa wa Mara ambapo walikutwa na nyavu za dagaa za milimita 6 ambazo ni kinyume na sheria.

Akizungumza na wananchi wa mwalo wa Sota Kata ya Tai wilayani Rorya, Novemba 7, 2018 Afisa Mfawidhi wa ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Ziwa, Didas Mtambalike alisema wavuvi kutoka nchini walikiwa wakishitikiana na wenzao kutoka Kenya kufanya uvuvi haramu kinyume na sheria ambapo walikutwa katika mtumbwi mmoja kuna kuna kuwa na watanzania watatu na mkenya mmoja au wskenya wawiki na watanzania wawili.

Didas alisema wavuvi hao kutoka nchini wamekutwa na makosa manne ikiwemo la kutumia nyavu haramu za dagaa za milimita sita, kutokuwa na leseni ya uvuvi, kutojisajili pamoja na kutumia taa za nishati ya jua (solar) ambazo haziruhusiwi katika Ziwa Victoria huku wakenya wakiwa wamefanya makosa kama ya wenzao ikiwa ni pamoja na kuingia nchini na kufanya shughuli za uvuvi bila kibali cha kufanya kazi nchini kutoka wizara husika.

Alisema,Sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, na kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na miongozo yake ya mwaka 2018 inakataza uvuvi wa kutumia zana haramu katika Ziwa Victoria, hivyo kutokana na kosa hilo watanzania watalipa faini ya milioni mbili kila mmoja huku wakenya wakilipa faini kwa mujibu wa sheria ya Tanzania,na mali zao ambazo ni Mitumbwi nane na injini nane kuendelea kushikiliwa na Serikali kisha kupelekwa kwenye vyombo vingine vya sheria kutokana na kuingia nchini na kufanya kazi bila kibali.

Pia alisema, kuna watanzania wachache wanaoendelea kushirikiana na wakenya kuwanyanyasa watanzania wenzao, hivyo anashangaa kuona tangu kuanza kwa oparesheni sangara januari bado kuna watu wanakamatwa kwa kosa la kutumia zana haramu za uvuvi, oparesheni hiyo itaendelea mpaka pale watakapojiridhisha kuwa uvuvi wa aina hiyo nchini umeisha na kila mwananchi ananufaika na rasilimali zilizopo ziwani hapo sanjari na kusisitiza kuwa haruhusiwi mtu yoyote kutoka nje ya nchi kufanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo upande wa Tanzania bila kibali na akibainika atawachukulua hatua za kisheria na kuwataka wavuvi nchini kuto vua upande wa nchi jirani bila kufuata sheria na vibali za eneo husika.

Hata hivyo Ofisa Mfawidhi wa Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Mara Jairos Mahenge alisema, watuhumiwa hao wapo kituo cha Polisi Wilaya ya Musoma huku akitoa wito kwa wananchi kushikamana na kuunga juhudi za Serikali kupitia oparesheni sangara na kila mmoja kuona uchungu kwa kutetea rasilimali ya nchini katika Ziwa Victoria kwa manufaa ya sasa na baadae.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Sota Shirati Ramadhani Said alisema, kuna watanzania ambao hawaitakii mema nchi ambao waliikimbia oparesheni hiyo kwenda nchi za jirani na ndio wanaoshirikiana na wavuvi wa nchi hizo kufanya uvuvi haramu ziwani hapo.

Naye mmoja wa wananchi wa Mwalo wa Sota Deus O'nditi aliipongeza zoezi hilo na kusema kuwa suala hilo ni uvunjivu wa sheria hivyo Serikali iwachukulie hatua ili kukomesha utumiaji wa zana haramu ziwani hapo na wavuvi nchini kuacha kushirikiana na wenzao kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.

No comments:

Powered by Blogger.