LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mradi wa Ustahimilivu Jijini Mwanza waleta matokeo chanya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience), unatekelezwa na taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, ukilenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na Majanga.

Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo, kuanzia mwezi Oktoba 2017 hadi Disemba 2018, wadau mbalimbali wamepewa mafunzo juu ya namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na majanga.

Aidha kupitia mradi huo, yamejengwa matenki mawili ya mfano kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B ambapo matenki hayo yamekabidhiwa leo, Disemba 21, 2018. Fuatilia BMG Online TV hapa chini kufahamu baadhi ya matokeo chanya ya mradi huu.
Viongozi mbalimbali wa taasisi binafsi na serikali wakifuatilia jambo wakati wa zoezi la kukabidhi matenki ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B zote za Jijini Mwanza, yaliyojengwa na taasisi ya Governance Links Tanzania kupitia mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience).

No comments:

Powered by Blogger.