LIVE STREAM ADS

Header Ads

"Tutawafuata popote wasiofuata sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini"- Biteko

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila wakitoka katika jengo la ofisi za mwekezaji wa hifadhi za wanyamapori ya Makao, Mwiba Holdings Limited kuelekea eneo linalosadikiwa kuendesha shughuli za uchimbaji hifadhini humo.
Baadhi ya wanyama wanaoonekana katika hifadhi ya wanyama ya Makao katika Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila na viongozi mbalimbali wakiwa katika eneo linaloonesha dalili za uchimbaji wa madini katika hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu.
Profesa Simon Msanjila akiwa na viongozi mbalimbali pori la Makao.
Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Eliaza Chilongani wakiwa katika hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Eliaza Chilongani akiongea jambo baada ya kupokea ugeni kutoka Wizara ya Madini.
Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Fredy Mahobe akizungumza jambo wakati wa kikao  baina ya ujumbe kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Eliaza Chilongani na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Meatu.

Na Nuru Mwasampeta 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo. 

Biteko aliyasema hayo Januari 05, 2019 alipofanya ziara ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. 

Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia. 

Aliendelea kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi hayo si kujiamlia tu. 

Biteko alisisitiza kuwa lengo la ziara hiyo si kutoa kibali kwa watu kuchimba katika hifadhi hiyo. “Sisi hatujaja kupromote watu wachimbe bali tumekuja kwa sababu watu wanachimba pasipo taratibu. 

Alibainisha kuwa ili mtu yeyote apate kibali cha kuchimba katika hifadhi hiyo sharti apate kibali kutoka mamlaka kuu nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji kwa sababu katika hifadhi hiyo kuna vyanzo vya maji, Mamlaka ya Mazingira (NEMC)pamoja na Wizara ya Madini. 

Katika ziara hiyo ya kushtukiza Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila aliyeelezea sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili mtu yeyote kuweza kujihusisha na shughuli za Madini. 

Aidha, Profesa Msanjila aliwataka watanzania kujua kuwa rasilimali madini zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya watanzania wote hivyo ni lazima wafuate utaratibu ili mapato yatokanayo na tozo mbalimbali kutokana na utafiti, uchimbaji na biashara ya madini ziwanufaishe watanzania wote. “Lazima niwaambie haya madini ni ya watanzania wote” alikazia. 

Akizungumzia chanzo cha taarifa ya kuwepo kwa uchimbaji katika hifadhi hiyo Leons Welenseile (Mjiolojia) alisema mnamo mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alifanya ziara iliyolenga kutatua mgogoro baina ya kampuni ya inayomiliki leseni ya uwindaji wanyamapori katika hifadhi hiyo Mwiba Holdings Limited na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo baada ya wananchi kutoridhishwa na kile walichokuwa wakikipata kutoka kwa mwekezaji huyo. 

Walipokuwa njiani kutoka katika kusuluhisha mgogoro huo ndipo wataalamu wa madini katika mkoa huo walikutana na loli lililobeba mchanga pasipokuwa na vibali halali vya kufanya uchimbaji huo nakubaini kuwa shughuli hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni hiyo ya mwiba kwa lengo la kukarabati barabara katika hifadhi hiyo pasipo kujua kuwa walipaswa kuwa na leseni ya kuchimba mchanga huo na kupigiwa hesabu iliyopelekea kulipa mrabaha wa milioni 50 baada ya kukiri kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani alikiri kutokuwa na taarifa za uchimbaji huo na kuwataka wataalamu na maafisa madini katika eneo lake kutoa taarifa pindi masuala ya ukiukwaji wa taratibu na sheria za nchi yanapotokea katika eneo lake ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto hizo.

No comments:

Powered by Blogger.