LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ziara ya RC Mongella visiwa vya Ukerewe yabaini mambo mengi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kulia), ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imekuwa na mafanikio makubwa. Ungana na BMG kung'amua yaliyojiri kwenye ziara hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameagiza ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanga kisiwani Ukara ukamilike na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaosoma katika Kata jirani ya Bukiko wahamie katika shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Bukiko kisiwani Ukara na kukagua ujenzi wa madara katika shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bukiko kisiwani Ukara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na msafara wake akikagua ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Bukiko ambapo Mongella ametoa mifuko 50 ya saruji ili kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella pia alikagua mradi wa umeme wa jua JUMEME katika kisiwa cha Ukara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua upanuzi wa Kituo cha Afya Murutunguru.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Murutungu (hawapo pichani). Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mwl. Balbina Joseph na kulia ni Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Colonel Magembe.
Afisa Elimu mkoani Mwanza, Mwl. Michael Ligola (kulia), akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Murutungu (hawapo pichani).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (aliyeinama), akifungua bomba la maji kama ishara ya uzinduzi wa mtandao wa maji katika Chuo cha Ualimu Murutunguru wilayani Ukerewe. Mwaka jana Rais Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uzinduzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Murutunguru na kuahidi kupeleka maji chuoni hapo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Murutungu kwenye uzinduzi huo. Mwaka jana Rais Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uzinduzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Murutunguru na kuahidi kupeleka maji chuoni hapo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Murutungu kwenye uzinduzi huo. 
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), alisema mtandao huo wa maji utasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Murutunguru ili wananchi pia wapate maji safi na salama.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali alioambatana nao akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru pamoja na waalimu wao.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.