LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Mwanza akutana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto waliosimama mbele), juzi amekutana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polled (wa tatu kulia waliosimama mbele) na kufanya nae mazungumzo ofisini kwake kuhusu ushirikiano uliopo baina ya nchini hizo mbili katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

Ujio wa Balozi Profesa Polled Jijini Mwanza unajiri wakati ambao tayari wataalamu zaidi ya 10 kutoka nchini Cuba wanatarajia kuanza kutoa huduma katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa Hospitali hiyo katika magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayopimwa kwa njia ya mionzi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati), akiwa katika mazungumzo na Balozi Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polled pamoja na ujumbe alioambatana tano.
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polled (katikati kushoto), akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), akimkabidhi Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polled (kulia), nakala ya mwongozo wa uwekezaji mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto waliosimama), akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polled (wa tatu kulia waliosimama). Wengine ni viongozi mbalimbali mkoani Mwanza akiwemo Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio (wa pili kulia waliosimama), Mkurugenzi Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Abel Makubi (wa kwanza kushoto waliosimama mbele) na wasaidizi wa Balozi Polled.

No comments:

Powered by Blogger.