LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella akagua ujenzi wa Hospitali ya Bwisya wilayani Ukerewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Na George Binagi-GB Pazzo
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella jana Januari 16. 2019 amekagua upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, kinachongengwa kwa hadhi ya Hospitali ya Wilaya.

Itakumbukwa kwamba Novemba 17, 2018 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alizindua rasmi ujenzi wa miundombinu katika Kituo hicho unaofanywa na kampuni ya SUMA JKT chini ya usimamizi wa Kamati Maalum iliyoundwa na Mongella kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 800.

Huu ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli aliyeagiza sehemu ya fedha za rambirambi zilizopatikana kufuatia ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichozama Septemba 20, 2018 zitumike kufanya ukarabati katika Kituo cha Afya Bwisya ili kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa kisiwa cha Ukara.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza akikagua ujenzi wa Hospitali ya Bwsya wilayani Ukerewe.
 Ujenzi huo unaendelea vyema na unatarajiwa kukamilika kwa wakati mwezi ujao.
 Hospitali ya Bwisya kisiwani Ukara inajengwa na kampuni ya SUMA JKT.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.