LIVE STREAM ADS

Header Ads

DUH SHUHUDIA "kumbe Aggrey Mwanri ana vipaji vingi"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

  Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika hii leo kwenye uwanja wa Kolimba, Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Mama Samia anaendelea na ziara yake ya siku tano mkoani Tabora iliyoanza Februari 21, 2019 ambapo leo akiwa wilayani Kaliua, amekagua na kuweka jiwe la ufunguzi kwenye jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Kaliua.

Pia amekagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya Kaliua. Pia amekagua na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Uyumbu kilichopo wilayani Urambo na baadaye kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye uwanja wa Kolimba, Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.