LIVE STREAM ADS

Header Ads

Fagio la Wizara ya Madini latua Tabora, Waziri Biteko azungumza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema Serikali kupitia wizara hiyo inatarajia kuzifuta zaidi ya leseni 50 za utafiti wa madini katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora, baada ya wamiliki wa leseni hizo kukaa nazo muda mrefu bila kuzilipia na kuzifanyia kazi.

Biteko alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa salamu za wizaya yake kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika Kata ya Simbo wilayani Igunga. Mama Samia ameanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Tabora kuanzia jana Februari 21, 2019.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.