LIVE STREAM ADS

Header Ads

GGML yafadhili ujenzi wa shule ya kwanza ya Umma ya Kiingereza mkoani Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Shule ya Bombambili ambayo ni ya Kwanza ya Umma ya Kiingereza Mjini Geita.
Wakati Tanzania inapiga hatua kuingia kwenye uchumi wa kati pamoja na Shirikisho la Afrika Mashariki,Taarifa zinaonyesha kuwa kuna haja ya Tanzania kuongeza vijana wenye uwezo wa kuzungumza kwa ufasaha lugha ya kiingereza ili kushindana vyema katika soko la ajira.
Wakati nchi zingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Historia walikwishaanza kutumia lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia masomo yote kwenye Shule za Msingi,nchini Tanzania shule nyingi za umma hazitumii kiingereza kama lugha kuu ya kufundishia masomo yote.

BMG Habari
Katika kutekeleza malengo ya kuwa na wahitimu bora na wenye sifa,elimu ya Msingi ina mchango mkubwa katika kutengeneza mustakabali wa wanafunzi kwenye lugha na ujuzi.

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Geita imewekeza Shilingi za Kitanzania Milioni 234 kujenga shule ya Umma ya Kiingereza katika eneo la Bomba Mbili Mjini Geita.

Makamu wa Rais wa Miradi endelevu ya GGML Bw Simon Shayo amesema, “Tukiwa Kampuni Raia,sisi kama GGML tumefanikiwa kuweka msisitizo kwenye kuboresha Elimu katika Mkoa wa Geita.

Katika Mpango wa Wajibu wa Kampuni kwa Jamii kwa mwaka 2018,tumefanikiwa kutenga kiasi cha fedha za kitanzania Bilioni 9.2 ambazo zaidi ya Bilioni 3.2 zimekwishapelekwa kujenga,kumalizia na kukarabati Shule za Msingi na Sekondari.Sehemu nyingine ya Bajeti imepelekwa kwenye Miradi ya Afya na miundombinu mingine ya kusaidia Jamii” alisema Bwana Shayo.

Akizungumzia maendeleo yaliyofikiwa kwenye ujenzi wa Shule hiyo ya Kiingereza ya Umma,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Apolinary amesema Shule ya Kiingereza ya Bombambili itapatiwa vifaa vya kisasa na miundombinu kuwasaidia wanafunzi mjini Geita na sehemu zingine.

Amewaomba Wazazi kuwapeleka Watoto wao kwenye Shule hiyo kwa mwaka 2019.Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Ada katika Shule hiyo pamoja na gharama zingine zimekwishapitiwa ili wazazi wengi waweze kuzimudu.

Mkuu wa Shule hiyo, Laurent Daniel amesema mpaka sasa jumla ya Wanafunzi 58 wamekwisha andikishwa katika Shule hiyo lakini malengo ni kuandikisha jumla ya Wanafunzi 320 kwa mwaka.

“Tunayo madarasa mazuri sita yaliyokamilika kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi.Kila darasa linaweza kuchukua wanafunzi hadi 40.Tunayo pia madarasa mawili kwa Wanafunzi wa awali na kila darasa linaweza kuchukua hadi wanafunzi 25. Ni matumaini yetu kuwa taarifa kuhusu ufunguzi wa shule hii itaendelea kufikishwa kwa Wazazi wengi zaidi ili tufikie lengo la kuandikisha wanafunzi wengi zaidi” alisema Mkuu huyo wa Shule.

Tangu kuanzishwa kwake, GGML imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na Serikali na wadau wengine kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii mkoani Geita kupitia mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi na mipango mingine ya kitaifa. 

Kwa kuongozwa na tunu yetu ya kuipatia Jamii ya Geita Miradi endelevu ya kijamii na kiuchumi,GGM inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii ya Mji wa Geita ikiwemo Mradi wa Maji Safi na salama kwa mji wa Geita,Elimu na shughuli za maendeleo ya uchumi kwenye Kilimo,ujenzi na sekta za huduma.

“Tunakusudia kuacha alama kwa wadau wetu katika Mji wa Geita na Tanzania kupitia uwekezaji wetu wa moja kwa moja,ajira tulizotengeneza,mapato tunayoyatoa kwa Serikali na kupitia uwekezaji endelevu tunaoufanya kwa Jamii wenyeji,” alisema Bw. Shayo na kuongeza;

Tutaendelea kufanya kazi na wadau wetu wote ili kuhakikisha faida endelevu ya uchumi inaendelea kupatikana kutokana na shughuli zetu za uchimbaji Dhahabu”. Kwa taarifa zaidi,Tembelea: www.geitamine.com

No comments:

Powered by Blogger.